*******************
SHIRIKA la Viwango Tanzania limeshiriki katika wiki ya maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu ambapo shirika limeendela kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za chakula zenye ubora na znazokidhi matakwa ya Viwango.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Afisa Usalama wa Chakula (TBS) Bw. Makaya Nsonda amesema ili kuwa na afya bora wazalishaji wanatakiwa kuzalisha bidhaa za chalula zilizokidhi matakwa ya viwango kwani kwa kufanya hivyo taifa litapata nguvu kazi kubwa kwani walaji wa bodhaa hizi hawataathirika na bidhaa hafifu.
Aidha ameongeza kuwa ni fursa kwa wajasilimali wa mkoani Simiyu na mikoa jirani kuweza kutembelea banda la TBS na kuweza kupewa elimu ya udhibiti ubora ili kuzalisha na kununua biidhaa zilizokidhi viwango .
“Ni fursa kwa wajasiriamali kuzalisha bidhaa na kuthibitishwa na TBS, kwaajili ya biashara ndani na nje ya nchi, kwani huthibitishwa na TBS bure”
Pia ameotoa wito kwa wajasirimali kutumia vyema fursa hii ya uthibitishaji ubora bure ili kuongeza thamani katika bidhaa zao chakula.