NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
MWAKILISHI wa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi.Neema Nyalege,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Chamwino Malick Mussa Maliki,akielezea lengo la Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT),Wilaya ya Chamwino Vicky Kibona,akisoma risala wakati wa Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino Dkt. Semistatus Mashimba,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
MKUU wa TAKUKURU Wilaya ya Chamwino Sipha Mwanjala,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
MKUU wa Fedha Utumishi wilaya ya Chamwino Abdull Mbimbi,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Deogratius Ndejembi,akipokea tuzo kwa niaba ya Rais Samia kutoka kwa Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Chamwino Malick Mussa Maliki,kwa kujali masirahi ya watumishi wakati wa Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Deogratius Ndejembi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Deogratius Ndejembi,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
……………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Deogratius Ndejembi, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino kushughulikia madai yote ya walimu na wastaafu kwa wakati.
Agizo hilo amelitoa jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Chamwino.
Amesema miongoni mwa mambo yanayodaiwa na walimu ni kulipwa pensheni kwa daraja la zamani.
“Imani yangu Afisa Utumishi wa Wilaya anajua utaratibu unaosimamiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na hatua za kuchukua kwenye suala hili, nimuagize Mkurugenzi wa Halmashuari yetu kushughulikia kikamilifu na kwa wakati,”amesema.
Amesisitiza kuwa serikali imeendelea kuhughulikia maslahi ya watumishi wa umma nchini wakiwemo walimu ambapo ndani ya mwaka mmoja na nusu wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, watumishi zaidi ya 200,000 wamepandishwa madaraja.
Ameagiza CWT kusimamia kikamilifu walimu wasiowajibika ipasavyo na kukiuka sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Awali, akisoma risala YA Chama hicho, Katibu wa CWT Wilaya ya Chamwino, Vicky Kibona, ametaja mambo saba kwa serikali mambo saba ikiwamo kuangalia upya kikokotoo cha mafao kwa kuwa kimepunguza mafao kwa walimu kutoka asilimia 50 hadi 33.
Pia Kibona amesema jambo jingine ambalo serikali inapaswa kushughulikia ni walimu kutopandishwa vyeo au madaraja kwa wakati hali inayowavunja moyo na ari ya kufanya kazi kwa bidii.
“Jambo jingine walimu wanaofikia hitimisho la kazi(wastaafu) mwajiri hawarejeshi makwao kwa wakati, matokeo yake wastaafu hawa huishi maisha ya kudhalilika kwa kukosa ahali pa kuishi ukizingatia wanakuwa wameshafukuzwa kwenye nyumba za shule,”amesema.
Katibu huyo amesema suala jingine ni madai mbalimbali ya mishahara na yasiyo ya mishahara yaliyohakikiwa Januari 2017 ambayo bado ni kero kubwa sana kwa walimu kwa kuwa hajalipwa hadi sasa.
“Miundombinu duni katika shule zetu yaani madarasa yasiyokidhi mahitaji, nyumba chakavu za walimu na maeneo mengine hakuna kabisa,”amesema.
Kibona amesema pia wastaafu kulipwa mafao kwa daraja la zamani badala ya jipya kwa kuwa mwajiri hajapeleka michango na tozo kwneye Mfuko wa Hifadhi ya Jami kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Kadhalika, amesema CWT inaomba muda wa kumaliza vipindi uangaliwe kwa kuwa umekuwa si rafiki kutokana na jiografia ya eneo hilo.