Iringa, Stanslaus Mhongole akiongea na walimu viongozi wa wilaya ya
Kilolo mkoani Iringa namna ya kutatua changamoto zaoNa Fredy Mgunnda, Iringa.
Chama Cha walimu ya Wilaya ya Kilolo
kimeiomba Serikali ya jamhuri ya muungano was Tanzania kuwajengea nyumba walimu
kwenye maeneo ambayo wanafanyia Kazi Ili kuongeza weledi wa Kazi kazini.
Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa
walimu Wilaya ya Kilolo, katibu wa chama cha walimu wilaya ya kilolo (CWT) wilaya ya Kilolo Anthony
Mang’waru alisema kuwa walimu wa Wilaya ya Kilolo Kwa asilimia kubwa
hawana nyumba za kuishi hivyo kupunguza hali ya utendaji wa Kazi Kwa walimu.
Mang’waru alisema kuwa serikali
imekuwa inafanya Kazi kubwa katika ujenzi ya vyumba vya madarasa na vyoo vya
shule lakini imekuwa ikisahau kujenga nyumba za walimu Kwa ajili ya kuishi
katika maeneo ya kazi Hali inayowalazimu waalimu wengi kuishi meneo ya mbali na
shule kutokana na kukosekana Kwa nyumba za waalimu.
Alisema kuwa walimu wanafanya kazi
Kwenye mazingira magumu kutokana na kukosekana Kwa miundombinu ya nyumba za
walimu kunakosababisha walimu kushuka Kwa molali ya walimu kufundisha
Mang’waru alisema kuwa baadhi ya shule ukabiliwa na magumu ikiwemo
ukosefu wa vyoo kwa ajili ya waalimu hali inayowalazibu kubisha hodi katika
makazi ya wananchi walio jirani na shule ambazo walimu hao wanafundisha
kwa uapande wake Mwenyekiti wa chama cha waalimu wilaya ya
Kilolo Mwl Mtemi Mgalula alisema kuwa walimuwa wanakumbana na hali ya
kustaajabisha, anasema hali ya miundombinu siyo ya kuridhisha kwani pamoja na
kuwapo kwa miundombinu chakavu zipo shule zisizo na madara na hata ofisi za
waalimu hivyo wanafunzi ulazimika kusomea chini ya mti kama ilivyo kwa waalimu
kutumia miti ilipo katika shule zao kuwa ofisi
Kiongozi huyo wa chama cha waalimu wilaya ya Kilolo Mwl Mtemi
Mgalula Alisema kuwa shule hizo zimegeuka adhabu kwa waalimu hali inayofifisha
morali wa ufanyaji wa kazi ya kufundisha huku akiiomba Serikali kuzipatia
ufumbuzi
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo ndiyo alikuwa Mgeni rasmi katika
mkutano huu mkuu wa chama cha walimu wilaya ya kilolo anasema tayari jitihada
za utatuzi wa changamoto hizo zinaendelea kwa kutumia nguvu za wananchi pamoja
na wafadhiri katika baadhi ya maeneo
Hata hivyo amewahimiza waalimu kuwa wavumilivu wakati serikali
inashughulikia changamoto hio huku akiwata wananchi wa kilolo kushirikiana na
serikali katika katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya shule ili
kuwawezwesha wanafunzi kuwa katika mazingira salama ya kujifunzia