*****************
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeliwezesha Jeshi hilo kufanya kazi zake kwa weledi, haki na uadilifu kwa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unazidi kuimarika.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, kamishna wa Utawala na Menejimeti ya Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba, wakati akifungua warsha ya siku tano inayofanyika mkoani Morogoro ya kuwajengea uwezo Makamanda wa Polisi wa mikoa, Wakuu wa Vikosi pamoja na baadhi ya Maafisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Polisi hasa katika eneo la mawasiliano ya kimkakati na uongozi.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Muslim amempongeza, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura, kwa jitihada za kuhakikisha maafisa wanapata mafunzo yatakayowajenga kwenye utendaji wao wa kazi za Kipolisi na kuwa na utendaji wenye tija na kuweza kutoa huduma bora kwa Watanzania.
Kwa upande wake Bwana William Kallaghe, ambaye ni msemaji wa IPRT (INSTITUTE OF PUBLIC RELATIONS IN TANZANIA) wanaoendesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na wadau wengine, amesema kuwa, mafunzo haya ni maalum kwa watendaji wa Jeshi la Polisi ambayo yamejikita katika stadi laini (Soft Skills) kwa kuwaongezea uwezo wa kiutendaji maafisa wa Jeshi hilo.