Mjasiriamali Saimon Sirilo.
Kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development linalofanya kazi na Vijana tumeshiriki katika
maadhimisho ya wiki la vijana na kuweza kubadilishana mawazo na vijana wengi wa
Kitanzania mkoani kagera kwa kuwajengea uwezo katika mambo kadhaa ikiwemo namna
ya kujiajiri,Afya na makuzi pia.
Kupitia mambo mtambuka yanayowahusu kujenga uchumi wa vijana nilifanikiwa
kuwa moja ya wanajopo walioendesha mdahalo uliojikita katika kuzungumzia hatma
ya uchumi wa vijana kupitia mafaniko,changamoto na mapendekezo kwa serikali.
Binafsi,nilitoa mawazo yangu kama ifuatavyo
1:Vijana kuwa na uthubutu na kuanzisha mambo/miradi japo kwa kidogo ili
kuweza kuiaminisha serikali kuwa vijana tunao uwezo,maarifa,nguvu na ari ya
kufanya kazi…hapa ndipo serikali itawashika mikono kupitia zile fedha
asilimia 4 za vijana kutoka halmashauri.
Uthubutu huleta kuaminika zaidi kuliko maneno matupu,kijana mwenye uthubutu
huaminika zaidi kuliko asiyeanza kabisa.
2: Vijana tujitahidi kutafsiri fursa
zinazotuzunguka katika jamii zetu ili kuifanya serikali ione fursa hizo zina tija katika jamii zetu na kutupatia
fedha kama mtaji.
Fursa zipo nyingi sana ila zinapaswa kutafsiriwa kwa umuhimu wake, mfano, jamii moja inaweza
ona fursa zaidi ya moja kwa kitu kile kile…Mti waweza kuwa na fursa nyingi
kadiri atakavyoutafsiri mtu,mwingine anaona mti ni fursa ya mbao, mwingine
fursa ya dawa,mwingine fursa ya
kiganga,mwingine fursa ya mazingira nk…hivyo ukienda kwa hoja hii ya tafsiri
na kuelezea faida yake utaaminika zaidi.
Fursa zipo nyingi sana ila zinapaswa kutafsiriwa kwa umuhimu wake na hapa
ndio hoja ya kusema vijana tubadili taaluma zetu kuwa fedha na ziendane na
matumizi ama mahitaji ya jamii husika.
*Changamoto zinazowakabili vijana na
kushindwa kufikia malengo yao*
1: Ukosefu wa mtaji,hii ni kutokana na kutumia muda mwingi masomoni na kurudi mtaani wakiwa hawana kitu
kabisa.
2: Jamii kuwa na kasumba y kutowaani kulingana na sifa za vijana wachache
kutoridhisha.
3: Vijana wasomi wamejengewa uwezo wa kuajiriwa zaidi kuliko
kujiajiri,jambo hili huwapa changamoto vijana pale wanapokosa ajira
walizozisotea kwa muda mrefu.Vijana wengi hujikatia tamaa ya kupambana baada ya
kukumbana na ugumu wa maisha.
*Mapendekezo*
1:Vijana waanzishe mawazo na kuunda vikundi wakapewe fedha halmashuri
pamoja na mfuko wa vijana kutoka wizara
inayohusika na vijana na watu wenye ulemavu ambapo hata kijana mmoja
mmoja huweza kukopesheka kwa masharti nafuu.
2: serikali iwaamini vijana na kuendelea kutengeneza miundombinu wezeshi
ili kuwawezesha vijana kufikia malengo yao.
3: serikali ibadili mfumo kwa wasomi wanaopata fedha za mkopo kwaajili ya
masomo yao basi ikifaa kiasi kidogo cha asilimia anachopata mnufaika basi
atunziwe ili punde amalizapo masomo yake akabidhiwe fedha yake na iwe kama
kiinua mgongo cha kumsaidia kuanza
biashara wakati akisubiria ajira na hii itamsaidia kuanza kurejesha huo
mkopo aliopewa chuoni.
Mfano, kama mtu amepewa mkopo asilimia 100 basi wakati wa masomo yake
akabidhiwe asilimia 80 kwa mwaka na asilimia 20 aitunziwe kila mwaka ili
amalizapo masomo yake akabidhiwe ili iwe kama mtaji wake wa kuanzia maisha
wakati anasubiria ajira yake kwani serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi sana
kwa wanafunzi lakn hazirudi kutokana na vijana hao kukosa ajira.
*Mwisho*
Sisi vijana tunaendelea kupambana na kujengeana uwezo sisi kwa sisi, pia
tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita chini ya mama samia kwa mambo
makubwa inayofanya kwa vijana kwa mustakabali wa Taifa letu na tupo bega kwa
bega na Mh. Rais kuhakikisha tunalijenga Taifa letu pendwa.
Imeandaliwa na SAIMON SIRILO
MJASIRIAMALI