Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo Bukoba Mkoani wa Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Chen Mingjian kuzindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo, Burugo kata ya Nyakato Bukoba Mkoani Kagera tarehe 13 Oktoba, 2022. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo, Burugo kata ya Nyakato Bukoba Mkoani wa Kagera tarehe 13 Oktoba, 2022. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Chen Mingjian, Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama cha Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea na kukagua moja ya Madarasa yatakayotumika na Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA), Bukoba Mkoani Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia na kupata maelezo ya mashine mbalimbali zilizopo kwenye moja ya karakana ya Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo, Burugo kata ya Nyakato Bukoba Mkoani wa Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Chen Mingjian kama ishara ya makabidhiano ya Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo, Burugo kata ya Nyakato Bukoba Mkoani Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua mashine mbalimbali zinazotumika katika Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo Bukoba Mkoani wa Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali mara baada ya kuzindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo, Burugo kata ya Nyakato Bukoba Mkoani wa Kagera