*******************
Na Silvia Mchuruza,
Bukoba, Kagera.
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh.Samia Suluhu Hassan ameziagiza halmashauri zote za mkoa wa kagera kuhakikisha zinatenga vizuri zile asilimia kumi za mikopo kwa vijana ili kuweza kuwawezesha vijana kujiajili na kuajili vijana wengine pindi watakapo maliza mafunzo yao ya ufundi.
Maagizo hayo ameyatoa wakati wa uzinduzi wa makabidhiano ya chuo kikubwa Cha veta kilichojengwa mkoani kagera katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba, kata nyakato Kijiji burugo ambapo amewataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na mkuu wa mkoa kusimamia maagizo hayo ili kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi na kuzalisha taifa lenye vijana imara.
“Tunafanya haya yote kwa ajili ya kupambana na kile alichotuachia baba wa taifa just ya kupambana na njaa,ujinga na maradhi sasa kupitia chuo hiki tayari tumepambana na adui ujinga kwa kuwawezesha vijana wetu kupata elimu bora”
Ameongeza kuwa kutokana na utafiti uliofanyika na kitengo Cha utafiti nchini mwaka 2021 asilimia 12 ya vijana hawana ajira kupitia chuo hiki na vyuo vingine vya veta nchi vitachangia kuondokana na changamoto hiyo kwa kuwapatia vijana elimu ya ufundi stadi.
Nae Waziri wa elimu sayansi na teknolojia mh.prof Adolf Mkenda amesema kuwa mpaka kukamilika kwa chuo hicho kimegharimu billion 22 za kitanzania ambapo chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 1500 ambapo wanafunzi wa kozi za mda mfupi watakuwa 400 na mda mrefu watakuwa zaidi ya 1000.
Ameongeza kuwa mpaka sasa wilaya zote nchi 139 zimejengewa vyuo na vyuo 77 vinamilikiwa na veta na vyuo 4 vipo ngazi ya mkoa ambapo amesema kupitia chuo hicho vijana sasa wajivunie kupata elimu iliyo bora.
Pia Barozi wa China mh.Chen Mingjian barozi wa China nchini Tanzania amesema China imejipanga kutoa ajira zaidi ya laki 8 ndani ya bara la Afrika na Tanzania ikiwemo.
“Chuo kitatoa mafunzo endelevu ya ufundi na kukuza vipaji Kwa vijana na kuwasaidia kupata mafunzo ya kazi ya moja Kwa moja” amesema Barozi.
Pia China inachangia sana maendeleo ya elimu nchini Tanzania ikiwemo ujenzi wa maabara kubwa nchi Tanzania na Afrika Kwa ujumla kwani China imejipanga kushirikiana na Tanzania ilifike katika uchumi wa Kati wa viwanda pia.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa kagera Mh.Albert Chalamila amewataka wananchi kutumia vizuri rasilimali zinazotengenezwa na serikali kwa ushirikiano wa mataifa mbalimbali ikiwemo taifa la China Kwa kuenzi juhudi hizo.
Ameongeza na kuwasisitiza zaidi wananchi kufanya kazi Kwa bidii na kuachana majungu na kupitia chuo kikubwa Cha veta kilichojengwa mkoani kagera kuwaleta wanafunzi katika chuo hicho kwani kipo Kwa ajili ya kuusaidia mkoa na mikoa mingine nchi.
Nao baadhi ya wananchi wameshukuru uwepo wa chuo hicho akiwepo bi Haida Moses amesema kuwa chuo hicho ni tunu kubwa kwa wananchi wa mkoa wa kagera na taifa kwa ujumla na kitasaidia kuondoa changamoto za kielimu kwa watoto wao wanaohitimu madarasa ya kawaida.
” Wazazi wengi tulikuwa tunakosa nauli za kuwasafirisha watoto wetu uenda Kwa kufika katika maeneo ya kupatia elimu lakini kupitia chuo hiki tunamshukuru rais wetu kwa kazi kubwa”alisema bi Haida.