Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Mussa Hassan Mussa kilichotokea Zanzibar leo tarehe 13 Oktoba, 2022.
Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Mussa Hassan Mussa ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika utumishi wa umma.
Rais Samia amemtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na msiba huo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Peponi. Amina.