Mratibu wa Tamasha la Michezo na Utamaduni la Watoto, Bi.Akanashe Mwanga akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 13, 2022 kuelekea siku ya Tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 16,2022 Bagamoyo mkoani Pwani. Mratibu wa Tamasha la Michezo na Utamaduni la Watoto, Bi.Akanashe Mwanga akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 13, 2022 kuelekea siku ya Tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 16,2022 Bagamoyo mkoani Pwani. Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Africaree, Bi. Angela Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 13, 2022 kuelekea siku ya Tamasha la utamaduni na Michezo la Watoto litakalofanyika Oktoba 16,2022 Bagamoyo mkoani Pwani.
********************
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Michezo na Utamaduni la Watoto, litakalofanyika Oktoba 16,2022, katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 13,2022 Bagamoyo mkoani Pwani, Mratibu wa Tamasha hilo, Bi.Akanashe Mwanga amesema Tamasha hilo linatarajia kushirikisha watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano hadi 15, ambao wataonyesha fani mbalimbali.
Amesema maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo yamekamilika kwa kiasi kikubwa kwani lengo ni kuendeleza vipaji vya watoto mjini hapa ili kuhakikisha wanafikia malengo yao waliojiwekea.
“Tumeandaa tamasha la watoto kuanzia umri wa miaka mitano hadi 15 litahusisha watoto 80 wa fani mbalimbali ambapo tunarajia mgeni rasmi atakuwa Rais Mstaafu, Dkt Kikwete na ushiriki ni bure kabisa”. Amesema
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Africaree, Bi. Angela Ngowi, amesema tamasha hilo litakua la aina yake kwani litashirikisha sanaa mbalimbali na michezo.
Alitaja baadhi ya sanaa zitakazoonyeshwa na watoto hao kuwa ni ufinyanzi, ngoma, kuchora, muziki, kuruka kamba, rede na michezo mbalimbali ambayo imekuwa na faida ikichezwa na watoto.
“Tunatarajia tamasha litakuwa la aina yake kutokana na maandalizi tuliyoyafanya, tunatambua vipaji vya vijana wanaotoka familia za kawaida, hivyo tumeamua kuwaendeleza kutokana na vipaji vyao,” Amesema
Aliongeza pia katika tamasha hilo wataendesha harambee kwa ajili ya kuchangisha fedha za kujengea shule ya vipaji itakayokuwa na uwezo wa kuchukua watoto wengi zaidi kutoka Bagamoyo na Tanzania nzima.