Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio (Kushoto) akimkabidhi nyaraka mbalimbali Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Maduhu Kazi wakati wa makabidhiano ya ofisi baada ya kustaafu utumishi wa Umma leo Oktoba 13, 2022. Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali waliopo katika Wizara hiyo. (Picha na Jeshi la Polisi)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio akisaini nyaraka za makabidhiano wakati wa hafla ya kumkabidhi ofisi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Maduhu Kazi baada ya kustaafu utumishi wa umma. Makabidhiano hayo yamefanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali waliopo katika Wizara hiyo. (Picha na Jeshi la Polisi)