**********************
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili nchini Nigeria, Sinach Joseph Egbu anatarajia kuongoza jukwaa la Festival of Praise linalotarajia kufanyika keshokutwa, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam pamoja na mwimbaji nguli hapa nchini John Lisu.
Akizungumza na Fullshangwe blog muandaaji wa tamasha hilo, Lisu alisema umahiri wa Sinach utafanikisha ujumbe wa neno la Mungu kuwafikia watanzania wote kupitia tungo zake na waimbaji wengine wa hapa nchini.
Lisu alisema Sinach atapanda jukwaani na wimbo wake uliokamata anga la muziki wa Injili duniani wa ‘Way Maker’ uliotazamwa na mashabiki zaidi ya milioni 200.
Lisu alisema waimbaji wa hapa nchini watakaomsindikiza mwimbaji huyo ni pamoja na yeye mwenyewe, Christina Shusho, Ambwene Mwasongwe, Pasta EPA, Kwaya ya Kanisa la Moravian, Ruach Worship Team (Kenya) na Kwaya ya Gospel Winners.
Aidha Lisu alitoa wito kwa waamini wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo ni mojawapo ya matukio muhimu ya kusifu na kuabudu yanayofanyika hapa nchini.
Pia alitoa wito kwa aliwaomba waamini wa makanisa mbalimbali hapa nchini kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ili kupata upako kwa njia ya nyimbo kuabudu ambazo zitawajaza imani zaidi katika kufanya mambo yanayompendeza Mungu.