Na Irene Mark
KAMPUNI ya Bima ya Assemble ikishirikiana na Wakala wa Bima Fortis, wamezindua huduma ya bima ya moto kwa wajasiriamali wa dogo ambayo gharama yake ni sh. 8,000 kwa mwaka.
Bima hiyo iitwayo Malkia ni maalum kwa wajasiriamali wadogo hususan wanawake, vicoba na vikundi mbalimbali vya kibiashara.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Oktoba 12,2022 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Assemble, Tabia Massudi amesema wameukuja na bima mkombozi kwa wajasiriamali wadogo wote hasa wanawake ili kiunga mkono jitihada za serikali za kila mtanzania awe na bima.
“Tunajua sekta ya bima haina muamko sana zaidi ni wale wanaokata bima kwaajili ya vyombo vya moto sisi tumekuja na hamasa tumeleta sokoni bima ya Malkia inayomsaidia mjasiriamali kupata bima ya moto kwa ajili ya biashara yake.
“Gharama ya bima hii itakayopatikana kote nchini ni sh. 8,000 kima cha chini ambapo mjasiriamali akipata janga la moto kwenye biashara yake anapata huduma nyingi ikiwemo usjauri baada ya majanga na hudima za matibabu.
“Kumuona hapa Kamishna wa Mamlaka ya Bima Tanzania ni jambo la faraja sana hii ni katika kutuhakikishia kwamba jambo hili ni jema na lina manufaa kwa taifa,” anasema Tabia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Fortis, Maryam Shamo anasema ujio wa bima hiyo inampa fursa mjasiriamali kupata gari la wagonjwa pindi moto unapitokea kwenye biashara yake.
Pia mjasiriamali anapata ushauri wa kiafya baada ya ajali, matibabu kwa wagonjwa wa kulazwa hadi sh. Milioni moja na kiasi cha sh. 10,000 kila siku kwa siku 30 iwapo kuna muathirika wa ajali ya moto.
“Niwatoe hofu huduma hii
Hata hivyo alisema licha ya kwamba bima inajulikana kama Malkia lakini kila mjasiriamali anufaika nayo awe mwanamke au mwanaume,” anasema Maryam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Dk. Balgnayo Saquare, amewapongeza Assemble na Fortis kwa ubunifu wenye lengo la kumsaidia mjasiriamali na kuliona janga la moto linalowapa hasara wajasiriamali kila uchao.
“Nimekuja maalum kushuhudia na kuwapongeza sana ninyi mmekuja na bidhaa inayojibu mahitaji ya wananchi hongereni sana naamini mtabuni huduma nyingine bora zaidi,” anasema Dk. Saquare.