Kaimu Mkurugenzi wa elimu ya juu,Dk Evaristo Mtitu akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha .
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo unaofanyika jijini Arusha wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zinazotolewa katika mkutano huo.
……………………………
Julieth Laizer, Arusha.
Arusha.Wizara ya elimu,Sayansi na Teknolojia imeiagiza bodi ya mikopo ya elimu ya juu(HESLB)kuboresha huduma ya utoaji wa mikopo ili kuondoa changamoto ya baadhi ya wanafunzi kusitisha masomo kutokana na kukosa ada.
Akizungumza jijini Arusha katika kikao kazi kati ya HESLB,Maofisa kutoka vyuoni na wawakilishi wa wanafunzi chenye lengo la kuweka mikakati ya kuhudumia dawati la wanafunzi ili liweze kuboreshwa zaidi,Kaimu Mkurugenzi wa elimu ya juu,Dkt. Evaristo Mtitu amesema uboreshaji wa huduma ya mkopo utasaidia kila mwanafunzi mwenye sifa kuweza kutimiza ndoto yake ya kupata elimu ya juu.
“Nitoe wito kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu kutumia mafunzo haya kama chachu ya kuleta tija na ufanisi katika upangaji na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi,”amesema Mkurugenzi huyo.
Dkt.Mtitu amesema serikali wakati wote inaweka mikakati inayosaidia upatikanaji wa fedha za kutosha ili kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji na wanaotoka kwenye mazingira magumu ya kiuchumi waweze kupata elimu ya juu.
“Na imani yangu wanafunzi wahitaji wa mikopo ya elimu ya juu watapata taarifa za kutosha na kwa wakati namna ya upatikanaji wa mikopo na mahitaji yanayotakiwa wakati wa kuomba mikopo,”amesema Dkt Mtitu.
Pia amesema baada ya mafunzo hayo HESLB ni vyema wakahakikisha walengwa wanapata taarifa stahiki na maelekezo ili wanapoombwa kusiwepo kwa manung’uniko yoyote kwa wanafunzi wenye uhitaji wa mikopo.
Mkurugenzi wa uchambuzi na upangaji wa mikopo kutoka HESLB,Veronica Nyahende amesema kakao kazi hicho kitatoka na maazimio ya uboreshaji wa huduma ya hutoaji mikopo ili kuweza kuwafikia walengwa wanaoshindwa kutekeleza vigezo vya uombaji wa mikopo.
Mmoja wa Ofisa mikopo kutoka Chuo kikuu SUA,Santina Bugenyi amesema changamoto inayowakabili ni baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu kuhairisha masomo kutokana na kukosa fedha ya ada yote hivyo anaiomba bodi hiyo kuweka mazingira ya upatikanaji wa mikopo na utoaji wa taarifa kwa walengwa.
Naye Kamishna wa mikopo wa vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini,Emmanuel Martine ameishukuru serikali kwa kutenga kiasi cha sh.573 bilioni kwa ajili ya elimu ya juu nchini na inakwenda kinufaisha zaidi ta vijana 640 hivyo ni matarajio yao huduma ya mikopo hiyo itaboreshwa na kuweza kuweka mikakati ya kudumu.