Na Silvia Mchuruza,Bukoba,Kagera.
Waziri wa nchi,vijana, ajira na wenye ulemavu Waziri Joyce Ndalichako amewasisitiza wananchi ndani ya mkoa wa kagera na hata nje ya mkoa wa kagera kuhakikisha wanajitokeza katika kilele cha mbio za mwenge kitaifa ambapo mwenge utazimiwa mkoani kagera.
Ameyazungumza hayo alipokuwa akikagua maandalizi ya siku hiyo ya kilele hicho cha mbio za mwenge ambapo sherehe hiyo itafanyika mjini bukoba katika uwanja wa kaitaba na kuridhishwa na maandalizi hayo ambayo yanategemewa kuhudhuriwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ambae ndiye atakuwa mgeni rasmi.
“kiukwel nimeridhishwa na maandalizi haya lakini pia tukumbuke iyo siku ya kilele cha mbio za mwenge ndiyo siku maarumu ya siku ya kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa kwaiyo wananchi mjitokeze kwa wingi katika siku hiyo muhimu”
Hata hivyo pia amesema kuwa siku hiyo serikali imeandaa ibada maarumu ya kumuenzi baba wa taifa itakayofanyika kanisa kuu la kikatoriki kathedro.
Aidha nae mkuu wa mkoa wa kagera mh. Arbert Chalamila amesema kuwa mpaka sasa mkoa wa kagera unao watu wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini hivyo amewataka wananchi ambao wanaofanya shughuri za uuzaji wa chakula kuhakikisha wanapika chakula kizuri hata upande wa maradhi pia.
kwa upande wao jeshi la polisi mkoa wa kagera nao wamesema kuwa usalama wa mkoa upo vizuri na shwari kila kona ya mkoa kwa ujumla.