Na Silvia Mchuruza,Bukoba,Kagera.
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya kupitia wiki ya vijana inayofanyika kitaifa mkoani Kagera katika viwanja vya gymkana imejipanga kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha Kwa jamii hasa vijana ambao ndio waathirika wakubwa katika matumizi ya madawa ya kulevya ili kuwakinga na uraibu wa madawa ya kulevya.
Hayo yameelezwa na kamishina msaidizi kitengo cha Kinga na Tiba dokt Cassian Nyandindi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda lake lilopo katika maonesho ya wiki ya vijana ambapo amesema kuwa mpaka sasa serikali imejipanga vizuri kuhakikisha udhibiti wa matumizi ya madawa ya kulevya Kwa vijana na hata jamii Kwa ujumla yanafanikiwa nakupungua kabisa.
Aidha ameongeza kuwa kundi kubwa la vijana kuanzia miaka 15 mpaka 35 ndilo kundi kubwa linaloathirika zaidi ambapo mpaka serikali imejitaidi kupambana japokuwa bado uuzaji wa madawa bado upo ijapokuwa unafanyika katika mazingira tofauti pia serikali inazidi kudhibiti njia hizo.
” Serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu upande wa kitengo cha Kinga na Tiba tunaendelea kudhibiti uraibu ambao unajitokeza ikiwa kazi yetu kubwa kama kitengo cha Kinga na Tiba ni kuhakikisha tunaisaidia jamii na kundi kubwa la vijana linaepukana na janga hili la urahibu na uathirikaji wa madawa ya kulevya”
Pia ameongeza kuwa ndaani ya kipindi Cha miaka mitano mpaka kufikia Mwaka 2021 serikali imeweza kudhibiti usambaaji wa Tani 176.05 za bangi ambapo Kwa Mwaka 2021 pekee ni Tani 22.75,mirungi tani 130.2 Kwa Mwaka 2021 pekee ni Tani 10.9, eroin kg 3311.9 Kwa Mwaka 2021 pekee kg 1124.5 , cocein ni kg 38.2 na upande wa kemikali bashirifu mpaka kufikia June 2022 ilidhibiti kg 122,066.9.