Na WyEST
Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania anatarajiwa kupokea na kuzindua Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera.
Halfa hiyo inatarajiwa kufanyika Alhamis tarehe 13 Oktoba, 2022. Katika Chuo hicho kipya kilichopo Burugo Nyakato Kagera.
Chuu hicho chenye karakana, vifaa na miundo mbinu ya kisasa kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya China kitakuwa na uwezo wa kuchikua wanafunzi zaidi ya 1,400 kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika fani mbalimbali za ufundi na huduma.
Hayo yameelezwa na Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokagua maandilizi ya halfa hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wa Mkoa wa kagera na mikoa mingine ya jirani kushiriki katika ufunguzi huo.
Ametumia nafasi hiyo pia kuwataka vijana kujiunga na mafunzo ambayo yanalenga katika kujenga ujuzi yatakayokuwa yanatolewa katika chuo hicho.