Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) Christine Mwakatobe,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za kampuni hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 11,2022 jijini Dodoma.
WAANDISHI wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) Christine Mwakatobe,akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za kampuni hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 11,2022 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) Christine Mwakatobe,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na a waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za kampuni hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 11,2022 jijini Dodoma.
……………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) Christine Mwakatobe,ametaja mikakati ya kampuni hiyo ni pamoja na kuongeza idadi kubwa ya abiria katika uwanja huo .
Hayo ameyasema leo Oktoba 11,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za kampuni hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mwakatobe ameitaja mikakati ambayo wanayo ni kuongeza idadi ya abiria na kukarabati eneo la uwanja ili kuchukua magari 200 kutoka magari 83 yanayoweza kuchukuliwa kwa sasa.
Amesema mpaka sasa mkataba wa ukarabati wa ujenzi huo umeshasainiwa na hivi karibuni ujenzi utaanza na utagharimu Sh bilioni 2.7.
Amesema tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo imelipa kodi kwa serikali zaidi ya Sh bilioni 6.
Amesema kampuni hiyo pia imetoa gawio kwa Serikali Sh bilioni 3 ambapo mwaka 2016/17 Kampuni ilitoa Sh milioni 555 mwaka 2017/18 ilitoa Sh milioni 583 na mwaka 2018/19 iliigawia serikali Sh bilioni moja.
Aidha amesema kuwa ongezeko la abiria kutoka laki 347,757 mwaka 2020/21 na kufikia abiria laki 654,159 mwaka 2021/22 ni sawa na ongezeko la asilimia 88.
“Filamu ya Royal Tour imeendelea kuleta matokeo chanya katika uwanja wa KIA nakusababisha ongezeko kubwa la abiria kutoka mataifa mbalimbali.”amesema Bi.Mwakatobe
Ametaja mafanikio mengine ni kupitia shirika jipya la ndege la Eurowings Discover(part of Lufthansa Group)iliyoanza safari zake kutoka Frankfurt,Ujerumani kwenda KIA kuanzia mwezi Juni mwaka huu,shirika hilo linachangia kuongeza idadi ya abiria na mizigo.
“Kuendelea kuwa na mashirika mbalimbali ya ndege za kukodi(charter flights)ambayo yameendelea kutumia KIA kwa kuleta makundi maalumu ya watalii kutoka sehemu mbalimbili duniani.”ameeeleza
Amefafanua kuwa :”Kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza KIA katika maeneo tofauti ikiwemo hotel za kisasa,maeneo ya biashara mchanganyiko na jengo la wageni mashuhuri.