********************
Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Wafugaji wa Jamii ya kimasaii waliohamia katika kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga wamesema wameamua kwa hiari yao wenyewe kuhamia Msomera kuunga Juhudi za uhifadhi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.
Wafugaji hao ambao wamehamia eneo hilo wakitoka katika mamlaka ya hifadhi Ngorongoro wamesema watalitumia eneo hilo kwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo tofauti na mwanzo walipokuwa katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo fulsa hiyo hawakuipata.
Hayo wamesema leo October 09 katika kijiji cha Msomera baadhi ya wafugaji Wa Jamii ya kimasaii mara baada ya kuwasili kwa kundi la kumi na mbili katika Kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, wafugaji hao wamesema wanamuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jitihada zake za kukuza ufadhi na utalii alizoanza kujionyesha katika Nchi yetu.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA amesema zaidi ya mifugo elfu kumi mia saba thelathini na nane wamewasili katika kijiji hicho ikiwa ni awamu ya kumi na mbili.
ACP PASUA amesema Jeshi hilo linaendelea kuwahakikishia wananchi wanaohamia katika Kijiji cha Msomera kuwa Mifugo yao iko salama ambapo amewataka kufuata matumizi bora ya ardhi ili kuepusha Migogoro ya wakulima na wafugaji.
Kamanda Pasua amebainisha kuwa zoezi la kuhamisha mifugo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro linaendelea kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Sambamba na hilo amewataka wafugaji wanao miliki silaha kinyume na utaratibu kuzisalimisha Jeshi la Polisi ili wawekewe utaratibu mzuri wa kuzimiliki kiharali ambapo amesema kuwa Muda wa msamaha wa africa umebakiwa na siku chache hivyo amewataka wajitokeze kusalimisha silaha ambazo wanamiliki kinyume na utaratibu.