********************
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Oct 9
Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete amewaagiza Watendaji wa idara ya ardhi nchini kutatua migogoro ya ardhi inayowakabili wawekezaji ikiwa ni sehemu ya kuwajengea mazingira rafiki ya uwekezaji, badala ya kuwa vikwazo.
Aidha amesema , dhamira ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuondoa changamoto mbalimbali za wawekezaji na wananchi wengine ikiwa ni pamoja na kupunguza kama sio kumaliza migogoro yao ya ardhi .
Ridhiwani aliyaeleza hayo wakati alipofika kutembelea Banda la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,SINOTAN,KINGLION katika Maonyesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara yanayoendelea katika viwanja vya standi ya mailimoja kibaha mkoani Pwani.
“Mwananchi anakuja anaonekana kuwa na tatizo linalohitaji usuluhishi lakini wewe Mtumishi badala ya kuwa suluhisho au kuwa njia ya kumtafutia jawabu la tatizo linalomkabili wewe nawe unakuwa sehemu ya ukwamishaji” alieleza Ridhiwani.
Alisema Wizara hiyo lazima iwe suluhisho la migogoro ya ardhi na sio kikwazo cha kuwaacha wakiteseka katika migogoro mbalimbali inayowakabili.
“Wewe Mtendaji lazima utoke uende kwenye maeneo ukaangalie ni jinsi gani unaweza kusuluhisha migogoro na ile ya jamii na wawekezaji, alisema Ridhiwani.
“Rais Samia ameifungua nchi kwa uwekezaji amekwenda nchi mbali mbali duniani kutangaza fursa za uwekezaji tulizonazo hapa nchini amewaita wawekezaji wamekuja nchini kuwekeza sasa kukiwa na migogoro itakwamisha juhud za Rais” Alisema.
Ridhiwani alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kuandaa Maonyesho hayo ambayo yametoa fursa kwa wawekezaji kutangaza bidhaa zao.
Katika hatua nyingine,alikabidhi hati za viwanja tano kwa wananchi waliokamilisha hatua zote za manunuzi mkoani humo.
Nae Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Pwani Hussein Idd alisema zaidi ya hati 150 zimetolewa kwa siku za maonyesho ya biashara yanayoendelea huku zaidi ya hati 300 zikiwa tayari zimekamika zilizokamilishwa.
Bilion 2.5 Chalinze kwa ajili ya upimaji wa ardhi wameweka mkakati wa kutoa huduma kwa wananchi wenye malalamiko.