Mratibu msaidizi wa Chanjo manispaa ya Iringa Betha Lyimo akiongea na waandishi wa habari kutoa taarifa ya hali ya wananchi ambao wamepata chanjo ya UVIKO 19 Manispaa ya Iringa
Mratibu
msaidizi wa Chanjo manispaa ya Iringa Betha Lyimo akiongea na waandishi
wa habari kutoa taarifa ya hali ya wananchi ambao wamepata chanjo ya
UVIKO 19 Manispaa ya Iringa
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
Zaidi
ya wananchi laki moja halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa, wamepata
chanjo ya ugonjwa wa UVIKO-19 sawa na asilimia 89 ya kuvuka lengo la serikali
la kuchanja asilimia 70 hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu.
Akizugumza
na wandishi wa habari wakati kutoa taarifa kwa umma kuhusu maendeleo ya chanjo ya
Uviko-19 katika Halmshauri ya Manispaa ya Iringa Kaimu Mganga Mkuu Manispaa
ya Iringa Dr Godfrey Mtunzi amesema kuwa hapo awali lengo lilikuwa ni kuchanja
watu 123,418.
“Toka
wameanza kutoa chanjo ya uviko 19 kwa wananchi manispaa ya iringa tumewafikia
wananchi 110,135 sawa na asilimia 89 na kunapenda kuwamiza wananchi waendelee
kupata chanjo ya uviko 19 kwa sababu ni salama kwa matumizi ya binadamu”,
alisema Mtunzi
Kwa
upande wake Dr. Clement Makoba Kutoka Hospitali ya Rufaa ya Iringa amesema kuwa
ni vyema wananchi wakapata chanjo ya uviko 19 ili kukamilisha asilimia 11
zilizobaki na kufikia asilimia mia ya watu waliopata chanjo.
Amesema
kuwa hawawezi kufanya majaribio kwa mwili watu kwa sababu chanjo hii ni salama
hivyo serikali inasisitiza wananchi kuendelea kuchanja ili kuepusha kupoteza
nguvu kazi ya Taifa.
Naye
Mratibu msaidizi wa Chanjo manispaa ya Iringa Betha Lyimo alisema kuwa bado
wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuchanja.
“Tumeendelea
kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo ya biashara maofisini, kwenye misikiti,
makanisani na katika makundi mbalimbali kuhamasisha chanjo na toka wamepata
chanjo hakuna madhara ambayo yameonekana kwa waliochanja” alisema Lymo.
Alisema
kuwa wameendelea kutoa chanjo ya uviko 19 kupitia Mkoba ambao unalengo la
kufika katika eneo ili kuwapatia chanjo wananchi ambao wanashindwa kufika
katika vituo vya afya.
Baadhi
ya Viongozi wa dini, Askofu Samuel shayo na Katibu wa Kadhi Mkoa wa
Iringa Ustaadh Abdallah Khalid Ndede wamesema kuwa wanashirikiana na waratibu
wa afya ngazi ya jamii kuwahamasisha waumini wao kupata chanjo ya Uviko-19 kwa
kuwa ni janga la kitaifa.
Walisema
kuwa katika mafundisho ya Dini wameamrishwa kuwaelekeza waumini wao kuchukua
tahadhari za kiafya endapo watakutana na majanga ya maradhi.