Na Mathias Canal, WEST-Mwanza
Serikali
imeitaka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Saalam (DIT) kuhakikisha kuwa
inaongeza ufundishaji kwenye ujuzi wa bidhaa za ngozi.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 7
Octoba 2022 wakati alipotembelea chuo hicho kampasi ya Mwanza ili kujionea
maendeleo ya taasisi hiyo ikiwemo mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha
Teknolojia ya Ngozi unaoendelea chini ya Kampuni ya Comfix Engineering.
Amesema
kuwa Serikali imetenga Shillingi Bilioni 19.6 kwa ajili ya ukarabati wa Taasisi
ya Teknolojia ya Dar es Saalam (DIT) Kampasi ya Mwanza utakaoleta mapinduzi ya
elimu kwa vitendo katika teknolojia ya ngozi nchini.
Prof.
Mkenda amesema serikali inafanya ukarabati huo katika mpango wake wa
kuhakikisha DIT inakuwa kitovu cha utoaji mafunzo ya ufundi wa utekengenezaji
bidhaa za ngozi ikiwa ni pamoja na viatu, mikanda, waleti, mabegi na mipira
jambo ambalo litasaidia kutengeneza ajira kwa vijana wengi kanda wa ziwa na
Tanzania kwa ujumula.
“Kupitia
DIT vijana wengi wanaweza kupata ajira, tunahitaji tuwe na vijana wenye ujuzi
kutoka kwenye chuo hiki wanaoweza kujiajiri na kuwa chanjo cha ajira kwa
wengine,” amesema Prof. Mkenda.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akitoa taarifa kwa Waziri
huyo ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha miundombinu
ya elimu ikiwemo ya DIT ambayo ni muhimu katika maendeleo ya sekta ya teknolojia
ya viwanda vya ngozi nchini.
Awali
Mwenyekiti wa baraza la DIT Mhandisi Dkt. Richard Masika akimkaribisha waziri
wa elimu katika taasisi hiyo amesema DIT imekuwa ikitoa mafunzo ya ufundi wa
utengenezaji bidhaa za ngozi kwa nadharia na vitendo ili kuwajengea uwezo
vijana wa waweze kushindana katika soko la ajira kitaifa na kimatafa.
“Kwa
sasa tunafundisha wanafunzi wetu utengenezaji wa bidhaa za ngozi kwa kutumia
mashine na mikono ili hata wakitoka hapa waweze kutejitengenezea ajira wao
wenyewe,” amesema Dkt. Masika.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ameanza ziara ya siku nane katika mikoa ya
kanda ya ziwa ambayo ni mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita na Kagera.