Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wataalamu mbalimbali wa Wizara za kisekta ambapo amesema jukumu la ulinzi wa shoroba ni letu sote.
Mkurugenzi wa Wanyamapori , Dkt, Maurus Msuha akizungumza kabla kumkaribisha Mkurugenzi wa Bunge na Siasa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Lina Kitosi kwa ajili kufungua kikao kazi cha wataalamu kutoka Wizara nane za Kisekta zilizokutana kwa muda wa siku mbili Jijini Arusha kwa ajili ya kujengeana uelewa wa pamoja katika kutekeleza mpangokazi wa kuongoa shoroba za wanyamapori nchini
Mkurugenzi wa Bunge na Siasa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Lina Kitosi akizungumz wakati akifungua kikao kazi cha wataalamu kutoka Wizara nane za Kisekta zilizokutana kwa muda wa siku mbili Jijini Arusha kujengeana uelewana wa pamoja katika kutekeleza mpangokazi wa kuongoa shoroba za wanyamapori nchini
Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, Dkt. Hamza Kija akitoa wasilisho kuhusu tathmini ya shoroba Wanyamapori nchini kwa Wataalamu mbalimbali kutoka wizara nane za kisekta
Baadhi ya Wataalamu mbalimbali kutoka wizara nane za kisekta wakifuatilia wasilisho kuhusu tathmini ya shoroba zawanayamapori nchini katika kikao kilichofanyika leo Jijini Arusha
Mkurugenzi wa Bunge na Siasa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Lina Kitosi akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha wataalamu kutoka Wizara nane za Kisekta zilizokutana kwa muda wa siku mbili Jijini Arusha kwa ajili ya kujengeana uelewa wa pamoja katika kutekeleza mpangokazi wa kuongoa shoroba za wanyamapori nchini
……………………………….
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi amesema ushirikiano kati ya Wizara za Kisekta ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha shoroba za wanyamapori haziendelei kuharibiwa
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Oktoba, 2022 wakati allipokuwa akizungumza kwenye kikao kazi cha Wataalamu waliokutana Jijini Arusha kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja na kujadili utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kuongoa Shoroba za Wanyamapori
‘’Jukumu la ulinzi wa shoroba za wanyamapori ni letu sote kwa maana ya Wizara zetu za kisekta ambazo zinagusa masuala ya Uhifadhi zikiwemo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi na Uchukuzi, Maji, Mazingira na nyinginezo ’’ amesema Naibu Katibu Mkuu, Mkomi
Amefafanua kuwa kikao kazi hicho cha Watalaam ni moja ya hatua muhimu itakayosaidia Wizara zinazohusika na uanzishwaji na usajili wa vijiji, ujenzi wa miundombinu, shughuli za kilimo pamoja ufugaji kuwa na uelewa wa pamoja katika kutekeleza mpango kazi wa kuongoa shoroba hapa nchini.
‘Kikao kazi hiki ni muhimu kwa kuwa kimewaleta wadau kutoka katika sekta mbalimbali mtambuka ambazo zina mchango wa moja kwa moja katika kuhakikisha shoroba za wanyamapori zinalindwa na kuhifadhiwa ‘ amesisitiza Mkomi.
Awali, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt.Maurus Msuha amesema kuwa jitihada za makusudi za kulinda shoroba zitasaidia kupunguza migongano iliyopo kati ya binadamu na wanyamapori hususani tembo.
‘Tunalinda wanyamapori hawa kwa ajili ya manufaa ya wananchi hivyo hatupendi kuona wananchi wanapata madhara kwa sababu tu wamejenga katika mapito ya wanyamapori hivyo ni lazima tuje na suluhisho la kudumu ili wananchi wasiendelee kupata madhara yanayoweza kuepukika” amesisitiza Dkt. Msuaha
Kwa upande wake,Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Bunge na Siasa, Lina Kitosi amesema kuwepo kwa shughuli za kibinadamu katika maeneo husika, kunasababisha wanyamapori wasiweze kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa migongano baina ya wanyamapori .
“Kuwepo kwa shughuli za kibinadamu katika maeneo husika, kunasababisha wanyamapori wasiweze kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa migongano baina ya wanyamapori na binadamu” amesisitiza