Mshindi wa mbio za Mita 3000 wanaume katika mchezo wa riadha kwenye mashindano ya Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Elibariki Buko kutoka Wizara ya Malisili na Utalii akimaliza mbio hizo zilizofanyika Oktoba 8, 2022 uwanja wa shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga jijini humo.
Mshindi wa mbio za Mita 3000 wanawake katika mchezo wa riadha kwenye mashindano ya Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Justa George kutoka Idara ya Mhakama Tanzania akimaliza mbio hizo zilizofanyika Oktoba 8, 2022 uwanja wa shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga jijini humo.
………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Tanga
WAKATI wanariadha Elibariki Buko wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Justa George wa Idara ya Mahakama wameibuka kidedea kwa kutwaa ubingwa wa mita 3,000 kwa wanawake na wanaume katika mchezo wa riadha uliofanyika kwenye uwanja wa Shule Sekondari ya Ufundi ya Tanga, timu zilizofuzu hatua ya 16 bora kwa michezo ya soka, netiboli na kuvuta kamba itachzwa Oktoba 9, 2022 kwenye viwanja vya Mkwakwani, Polisi Chumbageni, Bandari, Shule ya sekondari Popatlal, Usagara na Galanos.
Katika mbio hizo wachezaji walichuana katika mita 100, 200, 400, 1,500, 3,000 na kurusha tufe na zitaendelea katika hatua ya fainali itakayofanyika Oktoba 10, 2022 kwenye uwanja huo. Hata hivyo mita 1,500 na 3,000 zimemalizika.
Timu zilizoingia hatua ya 16 bora katika mchezo wa Kamba kwa upande wa wanaume timu zilizofuzu ni Idara ya Mahakama, Ofisi ya Rais Ikulu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST), Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maji, Hazina na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).
Timu mbili ambazo zitakazoshinda mchezo kati ya Ofisi ya Bunge, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zitaungana na timu nyingine katika hatua hiyo baada ya kufungana pointi.
Kwa upande wa wanawake timu zilizofuzu kwa hatua ya 16 bora ni Idara ya Mahakama, Wizara ya Maji, RAS Iringa, Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ofisiya Waziri Mkuu Sera, Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi); Hazina, Wizara ya Madini, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Wizara ya Mifugo na Uvuzi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Wizara ya Mambo ya Ndani na RAS Tanga.
Katika mchezo wa soka timu zilizoingia hatua ya 16 bora ni Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Ujenzi), Ofisi ya Bunge, wizara ya Mifugo na Uvuvi, wizara ya Katibu na Sheria, wizara ya Afya, RAS Simiyu, Hazina, Idara ya Mahakama, wizara ya Maji, wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, wizara ya Maliasili na Utalii, wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, RAS Manyara, wizara ya Kilimo na Ulinzi.
Aidha, Katika mchezo wa Netibali timu zilizoingia hatua ya 16 bora ni Ikulu, Wakala wa Hifadhi ya chakula ya taifa (NFRA), wizara ya Madini, Ukaguzi, Wizara ya Utamadunj, Sanaa na Michezo, Wizara ya Maliasili na Utalii, wizara ya Maji, Hazina, Wizara ya Afya, wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), ofisi ya Bunge, Ulinzi wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wizara ya Kilimo na Idara ya Mahakama.
Wakati huo huo, mbio za baiskeli kwa wanawake na wanaume zitafanyika Oktoba 9, 2022.