WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa,akizungumza kabla ya kuzindua na kukabidhi mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Faraji Mnyepe, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa kwa mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Majeshi nchini (CDF), Jenerali Jacob Mkunda,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo Mkakati, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akitoa taarifa ya Miradi ya JKT wakati wa hafla ya kukabidhiwa mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa (hayupo pichani) wakati akizungumza kabla ya kuzindua na kukabidhi mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa,akikata utepe kwa kuashiria uzinduzi wa mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 zilizokabidhiwa kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa,akiwa ndani ya trekta mara baada ya kuzindua na kukabidhi mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa,akipata maelezo mara baada ya kuzindua na kukabidhi mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma.
MUONEKANO wa Matrekta yaliyokabidhiwa
………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa,amezindua na kukabidhi mitambo na zana za Kilimo,zenye thamani ya sh.bilioni 3.9 kwa JKT zenye lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula pamoja na Usalama wa chakula nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dodoma Waziri Bashungwa amesema lengo ni kuongeza uzalishaji wa chakula hapa nchini pamoja na Usalama wa chakula.
Zana zizotolewa ni Trekta ambazo zimetoka nchini Italy zinauwezo wa kulima Heka 500 kwa siku,kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi,mashine za kupandia pamoja na za kuvunia.
Waziri Bashungwa amesema lengo la kufanya hivyo ni pamoja na kutaka kufanya uzalishaji wenye tija ili kuipunguzia serikali mzigo wa kusaidia chakula katika majeshi.
”Ili kufanikisha maendeleo ya kilimo ndani ya Jeshi hilo ni vyema wataalam wa kilimo wakatumika ipasavyo pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa kilimo na wizara.”amesema Waziri Bashungwa
Pia ameagiza JKT kuangalia na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao katika baadhi ya maeneo pasipo kutegemea mvua.
“Mitambo na zana za kilimo zinazonunuliwa ili ziendelee kutumika kwa muda mrefu ni vizuri kuwepo kwa matunzo na usimamizi wa karibu wa mitambo na zana husika,”amesema.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Faraji Mnyepe amesema miongoni mwa malengo ya bajeti ya JKT kwa mwaka 2022/2023 ni ukarabati na ujenzi wa miundombinu ili kuwezesha kuchukua vijana wengi zaidi katika shughuli za kulea kundi hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda ameliagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa katika mipango yake ya kilimo.
“Tunataka kwenda kuhakikisha tunatumia teknolojia ya kisasa katika kutekeleza malengo kwenye ufanisi wa tija zaidi,”amesema Jenerali Mkunda.
Pia ameiagiza JKT kuanzisha viwanda vya kimkakati ili kuendana na Sera ya Taifa.
Naye Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kwa nyakati tofauti wataendelea kununua mitambo na zana za kilimo ili kuwezesha lengo hilo kutimia.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo Mkakati, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema lengo ni kuhakikisha kuwa itakapofika mwaka 2024/2025 JKT inajitegemea kwa zana na mitambo na kuzalisha chakula cha kutosha na kuhakikisha usalama wa chakula unafikiwa nchini.
”Tumenunua matrekta makubwa 25 pamoja na zana zake zikiwa ni majembe ya kulimia, zana za kupandia na kuweka mbolea, kunyunyizia viatilifu na kuvunia mazao.”amesema
Brigedia Jenerali Mabena amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanafanya kilimo chenye tija ili kuhakikisha Jeshi hilo linajitosheleza kwa chakula.