**********************
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amefungua rasmi Mkutano wa 65 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani-Kamisheni ya Afrika (UNWTO-CAF), leo 5 Oktoba, 2022 jijini Arusha.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ” Rebuilding Africa’s Tourism Resilience for Inclusive Socio-Economic Development” umekutanisha washiriki takribani 200 kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayogusa shughuli za utalii barani Afrika.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeshiriki kikamilifu kwenye ufunguzi huo wa mkutano ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mej.Gen ( Mstaafu) Hamis Semfuko na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Mabula Misungwi Nyanda.