********************
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Kampuni ya Kinglion inayojihusisha na uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za mabati , Zegereni Kibaha,kina uwezo wa kuzalisha hadi mita 150,000 kwa mwaka kulingana na mahitaji.
Wakijinasibu katika maonyesho ya wiki ya biashara na uwekezaji Kibaha Mkoani Pwani,Ofisa masoko wa Kiwanda John Maduka alieleza ,ni kiwanda kinachokabiliana na ushindani wa soko la mabati ya kisasa ndani na nje ya nchi.
Alieleza ,kupitia maonyesho hayo watajitangaza zaidi na wanatarajia kupata soko zaidi ya ilivyo Sasa.
“Kupitia maonyesho haya ,Tunashukuru mkoa wa Pwani,kwani licha ya Kuwa na wateja Lakini tulikuwa bado hatujapanua wigo wa kujulikana zaidi ,Lakini kupitia maonyesho haya tunaamini tutapata wateja zaidi ya kipindi cha nyuma”kwani bidhaa zetu ni Bora “alisema
Maduka alifafanua ,Kinglion ni Kampuni inayokuwa kwa Kasi ndani ya Afrika Mashariki,kwa kipindi cha muda mrefu wameweza kudumisha ubora na unafuu wa bei.
Vilevile imeweza kutengeneza mawakala wengi katika mikoa yote ya Tanzania ,kwa kuunda uhusiano wa kuaminika kupitia huduma bora.
Maduka alielezea kwamba, mabati yanayopatika Kinglion ni pamoja na bati za rangi za kawaida pamoja na bati aina ya vigae,ambazo zipo katika muundo wa IT4,IT5,milano,Torino na Mkunjo.
Alisema Kampuni hiyo inatumia teknolojia ya kisasa na uwezo wa kuzalisha hadi mita 150,000 kwa mwaka.
Maduka alibainisha Kuwa ,Kampuni hiyo imepanua wigo wa kuhudumia wateja katika viwanda vidogo ilivyovianzisha Dar es Salaam,Arusha ,Mwanza,Mbeya,Dodoma na Zanzibar huku wakiwa na mpango wa kuongeza viwanda Burundi,Kenya ,Congo,Zambia,Uganda,Ethiopia na Kusini Mwa Sudan.