Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Stella Kiyabo,akizungumza leo Oktoba 5,2022 jijini Dodoma wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Stella Kiyabo,akifafanua jambo kwa walimu wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya utendaji Taifa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bakari Mtembo,akizungumza wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT),Wilaya ya Kondoa Ester Ntombola,akizungumza wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
KATIBU Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Dodoma Luya Ngonyani,akieleza jambo wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
MAKAMU Mkuu wa Chuo cha Ualimu Bustanu Emmanuel Muwanga,akitoa mada wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
SEHEMU ya walimu wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
MWAKILISHI wa Walimu Vijana wilaya ya Chemba Halidi Kunchili,akichangia mada wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
MJUMBE wa Kamato ya Utendaji Dodoma jiji Neema Mkobalo,akitoa mawazo yake wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
KATIBU Kitengo cha Walimu wanawake Wilaya ya Chamwino Judith Leon,akichangia mada wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
MWAKILISHI Shule za Msingi Wilaya ya Kondoa Mwalimu Deus Bwahama,akichangia mada wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
AFISA huduma na Utetezi CWT Makao Makuu Alfred Alexande,akichangia wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
MWENYEKITI CWT wilaya ya Bahi Hosea Maagi,akizungumza wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
MWENYEKITI CWT wilaya ya Chamwino,akichangia mada wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
MWENYEKITI CWT Dodoma jiji Prosper Mutungi,akizungumza wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
KAIMU Mkuu Idara ya Afya na Usalama Nelea Nyang’uye,akichangia wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya utendaji Taifa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bakari Mtemboakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
……………………………………
Na Alex Sonna-KONDOA
Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Stella Kiyabo,ameiomba Serikali kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyowakabili walimu nchini.
Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 5,2022 jijini Dodoma wakati wa kongamano la siku ya walimu duniani ambapo kimkoa limefanyika katika Chuo cha Ualimu cha Bustani kilichopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Amesema kuwa serikali inaajiri mwalimu lakini anapelekwa eneo la kwenda kufundisha hata nyumba ya kuishi hakuna pamoja na mazingira mabovu hali inayoathiri ufundishaji wake.
“Tunaona serikali inajenga madarasa kweli tunapongeza dhamira yake lakini kasi hiyo iende sambamba na nyumba za walimu, tumesikia itajenga mwaka huu wa fedha nyumba 809 bado ni ndogo, tunaomba tupewe kipaumbele”amesema
Aidha ametaja Vikwazo vingine ni kutokuwa na posho ya kufundishia na mishahara mizuri hali inayosababisha wawe na mikopo mingi inayowaumiza na kuathiri utendaji kazi wao.
Amesema kutokuwapo na mafunzo kazini yanayoendana na mabadiliko ya mitaala kumechangia kuwa na baadhi ya walimu wanaofundisha Tehama wakiwa hawawezi kuwacha komputa
Pia ameiomba Serikali kufanyika mabadiliko kwenye mwongozo wa usajili wa shule kwa kuweka nyumba ya mwalimu kama kipengele muhimu kwa shule kusajiliwa.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya utendaji Taifa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bakari Mtembo, amewataka walimu kuondoa unyonge kwenye kupambania haki zao na kutokubali kurudi nyuma.
“Msifanye haya tunayodai ni ya viongozi hapana tupambane wote ili yafanyike yataleta tija kwenye ufundishaji wetu, maana mwaka 2012 tulipotaka kugoma tuliambiwa mtakosa sensa tukatulia huo ndo ukweli,”amesisitiza
Aidha amesema kuwa CWT inaiomba serikali kurejesha posho ya kufundishia ili kufidia muda wa ziada ambao mwalimu anautumia kufanya maandalizi.
“Walimu walio wengi wameendelea kufanya kazi bila kupata mafunzo yoyote kazini ili kuboresha taaluma yao, yametokea mabadiliko ya mitaala lakini yalizingatia kubadilisha vitabu na kusahau kumpa maarifa mapya mwalimu ambaye ndiye kiini cha utoaji elimu”.amesema