Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Asasi ya Msaada wa Kisheria (LSF) Lulu Ng’wanakilala kuhusu machapisho mbalimbali yanayotolewa na Asasi hiyo katika wa Maonesho ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma , Oktoba 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mtoto mwenye ulemavu Chipowenga Zayeye, wa pili kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima na wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Brenda Msangi, katika wa Maonesho ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, Oktoba 4, 2022 Dodoma (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Doroth Gwajima Tuzo kwa niaba ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Oktoba 4, 2022. Katikati ni Mwenyekiti Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Mwantumu Mahiza kulia ni Mwenyekiti wa NaCONGO, Dkt. Lilian Badi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Oktoba 4, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)