Home Biashara WAZIRI DKT. BITEKO KATIKA BANDA LA BoT MAONESHO YA MADINI GEITA

WAZIRI DKT. BITEKO KATIKA BANDA LA BoT MAONESHO YA MADINI GEITA

0

Meneja wa Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi Victoria Msina (Kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko (Kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea Banda la Benki kuu ya Tanzania katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Bombambili mkoani Geita. Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela.

Afisa wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Miriam Mgina akitoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la BoT ili kupata elimu ya masuala mbalimbali ya Benki hiyo Katika maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye Viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita.

Afisa wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bi Rukia Muhaji akitoa elimu juu ya majukumu ya DIB kwa wanafunzi waliotembelea Banda la BoT katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Afisa wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi Rosemary Palagha akitoa elimu kwa mkazi wa Geita alitembelea banda la BoT katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Afisa wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Michael Mpiri akifundisha wanafunzi waliotembelea banda la BoT alama za utambuzi wa noti halali za kitanzania.

Afisa wa Benki Kuu ya Tanzania, Amon Mwambonda akitoa elimu kwa mkazi wa Geita aliyetembelea banda la Benki kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.