MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),Mhandisi Victor Seff,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 3,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za wakala huyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
WAANDISHI wa habari wakifatilia hotuba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),Mhandisi Victor Seff, (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za wakala huyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 3,2022 jijini Dodoma.
MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari -MAELEZO Bw.Gerson Msigwa,akizungumza mara baada ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),Mhandisi Victor Seff,kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za wakala huyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Octoba 3,2022 jijini Dodoma
……………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),Mhandisi Victor Seff,amesema kuwa wameimarisha miudombinu ya barabara za wilaya kutoka asilimia 15 mpaka asilimia 25 kwa sasa.
Hayo ameyasema leo Oktoba 3,2022 Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za wakala huyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mhandisi Seff amesema kuwa kwa sasa hali ya mtandao wa barabara za Wilaya kwa sasa ni asilimia 25, ambapo kilomita 34,056 ambayo ni sawa na asilimia 23.6 una hali nzuri, kilomita 48,684.36 sawa na asilimia asilimia 33.7 una hali ya wastani na Kilomita 61,689.42 ambayo ni asilimia 42.7 una hali mbaya.
“ Takwimu zetu zinaonesha kuwa asilimia 75.67 ya mtandao wa barabara za Wilaya ni za udongo na zinaathirika sana wakati wa misimu ya mvua na kusababisha maeneo mengi kutofikika. “
“ Mipango ya TARURA ni kuhakikisha inaboresha mtandao wa barabara za Wilaya angalau ziweze kupitika misimu yote.”
Aidha Mhandisi Seff amesema kuwa ili kupunguza gharama katika kukamilisha mirada mbalimbali za ujenzi wataweka kipaumbele katika matumizi ya malighafi zinazopatikana maeneoya kazi.
“Hadi sasa tumejenga madaraja 110 yenye thamani ya Shilingi bilioni 5 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50. Madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 72, Singida 13, Tabora 3, Kilimanjaro 6, Mbeya 2, Arusha 4, Mrorgoro 2 na Iringa 9,”Amebainisha Seff
Mhandisi Victor amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Wakala hiyo na kuanza majukumu yake mnamo Julai 1,2017 na kukamilika tarehe 30 June 2021 jumla ya Shilingi 1,297.79 milioni fedha za ndani zilitumika.
Ambapo Katika kipindi hicho jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 24,979.24 zilifanyiwa matengenezo, kilometa 955.35 zilijengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 16,857.82 zilijengwa/karabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Aidha, jumla ya madaraja 231 (kutoka Madaraja 2,960 hadi 3,191) na Makalvati 1,325 yamejengwa (kutoka Makalvati 67,992 hadi 69,317)
Katika kipindi hicho jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 24,979.24 zilifanyiwa matengenezo, kilometa 955.35 zilijengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 16,857.82 zilijengwa/karabatiwa kwa kiwango cha changarawe.
Ambapo jumla ya madaraja 231 (kutoka Madaraja 2,960 hadi 3,191) na Makalvati 1,325 yamejengwa (kutoka Makalvati 67,992 hadi 69,317).
Amesema mpango mkakati wa pili wa TARURA wa 2021 mpaka 2026 umepanga Kuondoa vikwazo kwenye mtandao wa barabara za Wilaya ili ziweze kupitika misimu yote,Kupandisha hadhi (upgrading) barabara za udongo kuwa za Changarawe/Lami kwa kuzingatia vipaumbele vya kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari katika majiji, manispaa na miji.
Mhandisi Victor Seff ameongeza kuwa kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2026/27 lengo la TARURA ni kuwa mtandao wa barabara za lami utaongezeka kwa km 1,450.75 (kilometa 2,404.90 – 3,855.65), changarawe km 73,241.57 (kilometa 29,116.57 – 102,358.14) na madaraja 3,808 (toka 2,812 hadi 6,620) ambapo fedha zitakazotumika kwenye mpango huu zinakadiriwa kuwa Zaidi ya Shilingi trilioni 4.2.
“Lengo la Mpango Mkakati wetu wa pili ni kuwa ifikapo 2025/26 asilimia 85 ya mtandao wa barabara za Wilaya chini ya TARURA zitakuwa zinapitika kwa misimu yote na nyakati za mvua hapatakuwa na taharuki inayojitokeza sasa kwa maeneo mengi kutofikika,”Amesema Mhandisi Seff
Mhandisi seff amesema kwa Mwaka wa fedha 2022/23 ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa pili ambapo TARURA imetengewa bajeti ya jumla ya Shilingi bilioni 838.16 ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 776.63 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 61.53 ni fedha za nje.
Naye Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Gerson Msingwa amesema katika kipindi cha miaka miwili, Serikali imezipelekea TARURA na Tanroadh kiasi cha Sh trilioni 4.7 kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya barabara.
“Nia ya serikali ni kuifanya nchi ifunguke na kufikika kila eneo na hilo linawezekana hata ukiangalia bajeti zinazelekezwa huko TARURA ni nzuri sana hivyo itawasaidia katika kukamilisha mipango yao na naamini kwa mikakati hii hakuna haja ya kuwa na wasiwasi nchi itafikika na itasaidia kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi kwa ujumla,”Amesema Msigwa