Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Kibaha Mjini (mstaafu),Mwajuma Nyamka amemwaga ,aliyekuwa akitetea kiti Cha Mwenyekiti CCM Kibaha Mjini,Bundala Maulid Bundala kwa kupata kura za kishindo 346 .
Bundala ameng’olewa kwenye kiti hicho ambacho alikitumikia kwa miaka 15 hivyo Nyamka kuweka rekodi mpya ya Mwanamama kushika nafasi ya Kuwa Mwenyekiti Kibaha Mjini.
Mwajuma alikuwa na wapinzani wake watatu ambao wote ni manguli wa siasa Bundala aliyepata kura 172,Sauda Mpambalioto aliyepata kura 33 na Abdallah Mdimu kura 32.
Baada ya kutangazwa Kuwa mshindi , katika mkutano mkuu wa CCM Kibaha Mjini ,Mwenyekiti mpya Mwajuma Nyamka alieleza mikakati yake ikiwa ni pamoja na kujenga umoja, kuimarisha mahusiano baina ya Chama na Serikali.
Nyamka aliwataka wanachama wa CCM kuvunja Makundi baada ya uchaguzi na kusisitiza upendo na mshikamano ili kusonga mbele ndani ya Chama.
“Uchaguzi umeisha, naomba makundi yaishe ,tuimarishe umoja na kujenga mshikamano kwa mstakabali wa Chama chetu”
Nyamka pia alikemea tabia ya kuwabughudhi viongozi waliochaguliwa wakiwemo wabunge na madiwani kuwaacha wafanye kazi zao pasipo kuwaletea vurugu
“Hatutosita kuwachukulia hatua za kimaadili wale watakaowabughudhi viongozi wetu,tuwaache wafanye kazi zao kwa mujibu wa taratibu Hadi watakapomaliza muda wao ,na Mimi nitakuwa mkali katika hili”alisisitiza Nyamka.
Wakati huo huo, Katika uchaguzi wa CCM Kibaha Vijijini ,Mkali Kanusu ameshinda kwa kupata kura 305 dhidi ya
wagombea wenzake Angolile Mwakajinga aliyepata kura 235, Amina Kobo 05 na Athuman Zanda kura 04.
Mjumbe kuwakilisha Taifa ameshinda Hamoud Jumaa kwa kupata kura 298, Abdallah Macho kura 209 na Seif Kachume 222.