Pia aliwatangaza Pendo Zelemani na Juma Mashaka kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa,wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa walichaguliwa Francis,Halima Nassoro na James Ling’wa.
Aidha makundi maalumu walichaguliwa Hadija Mfaume,Neema Ernest,Angelina Costantine na Rose Jacob (UWT),huku Matesa Richard na Dismas Masunu (Wazazi),Yusuf Salehe,Nelson Anderson,Kisari Simba na Jenisia Joseph (Vijana).
Begga akizungumza baada ya kutangazwa mshindi aliwashukuru wajumbe kwa kuchagua viongozi bora waliopanga kuwachagua baada ya kampeni kwa sababu Mungu amekubali wawe viongozi na kwamba kura 394 alizopata analo deni la kuwatumikia na ataendeleza alipoishia mtangulizi wake.
“Nawashukuru mmefanya uchaguzi wakisayansi na haikuwa kazi rahisi kwa sababu kila mgombea alikuwa akiwafahamu watu wake waliokuwa wakimwunga mkono, wagombea wote wamekubali matokeo na kusaini,”alisema
Pia alimshukuru mwenyekiti aliyemaliza muda wake kuwa, amefanya kazi kubwa nzuri,alikuwa kiongozi shupavu na kuahidi kumwomba ushauri kwa maslahi ya Chama.
Mwenyekiti huyo mpya alisema chama chochote cha siasa dhamira yake ni kushika dola na kusistiza kuwa makundi yaliyokuwepo wakati wa uchaguzi, baada ya uchaguzi kumalizika yote yavunjwe na kurudi ndani ya CCM moja kwa kazi moja iliyobaki ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Kuu 2025.
“Metuamini tuwatumikie 2024, hivyo tutangalia namna ya kutengeneza safu ya utendaji wa viongozi wetu,kwa sababu tumebaki na jukumu moja la uchaguzi wa wenyeviti wa serikali za mitaa 2024, pia uchaguzi mkuu 2025 tuhakikishe Mama yetu kipenzi, Rais Samia Suluhu Hassan anapata kura nyingi za kishindo ili kumtendea hiki,”alisema Begga.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM Nyamagana, Geofrey Kvenga alisema wajumbe walimaliza kazi yao kwa sababu uchaguzi wa Wilaya ya Nyamagana ni dira ya Mkoa wa Mwanza,hivyo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wilaya zingine.
“Nyamagana tumefanya uchaguzi huru na haki, wajumbe wamefanya maamuzi sahihi kwa kuchagua wagombea waliona wanafaa,naamini kwa Mkoa wa Mwanza tumeonyesha dira ya uchaguzi wa mwaka huu,kila mgombea alipita kujinadi na walipimwa kwa kiwango kikubwa na wapiga kura,hivyo Mungu ndiye hupanga nani awe kiongozi,”alisema.