MWENYEKITI wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
MSAJILI wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NGO), Vickness Mayao,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC),Onesmo Olengurumwa,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
MRAJISI wa asasi zisizo za kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdalla,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
MKUU wa Dawati la Wanachama THRDC Lisa Kagaruki,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO) Bi.Lilian Badi ,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini uliofanyika leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma.
……………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
MWENYEKITI wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza,ameyataka mashirika kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali ili kuondoa dhana iliyojengeka kuwa Asasi za kiraia ni adui wa serikali.
Hayo ameyasema leo Octoba 2,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali nchini.
Amesema kuwa mashirika yanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na Serikali ili kuondoa dhana inayojengeka kuwa Asasi za Kirai ni adui wa Serikali na hakuna maelewano
“Hapo zamani ilijengeka kuwa Asasi za kiraia ni adui na serikali jambo hilo siyo sawa kwani wote kila tunachokifanya ni kwa ajili ya maslahi ya taifa letu hivyo tunajenga nyumba moja hatipaswi kuogombania fito”amesema Mahiza
Aidha ameyataka mashiriki kutoyatumia mapungufu yalipo katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na serikali kama fursa ya kupata fedha kwa wafadhiri.
“Leo hii tumefika mahala tunavuana nguo ili tupate fedha kwa wafadhiri nawaombeni kama shirika linabaini kuna changamoto fulani basi kuwasailiana na uongozi wa eneo husika ili zifanyiwe kazi badala ya kupiga picha na kutuma huko duniani”amesema
Hata hivyo ameonya mashirika ambayo yatajihusisha na kutetea ndoa za jinsia moja kinyume na mila za kitanzania kwa madai ya kulinda haki za binadamu.
“Hatuwezi kuruhu haki za binadamu zinazopingana na mila zetu hata mara moja leo hii hata wewe mwanao wa kiume unasikia anaolewa na mwanaume mwezake utajisikiaje”?alihoji Mwantumu Mahiza
Kwa upande wake MRAJISI wa asasi zisizo za kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdalla,amewataka washiriki wa mkutano huo kutumia fursa hiyo kujadiliana changamoto zilizopo kwenye jamii na kuzifanyia kazi.
Naye Mkurugenzi wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa ameiomba serikali kufanyia marekebisho ya sera inayosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa ni pamoja na kuyaondolea kodi katika vitu mbalimbali ambavyo wamekuwa wakiingiza kutoka nje ya nchi.