NA
MWANDISHI WETU, DODOMA
MADAKTARI
nchini wametakiwa kuzingatia uadilifu, umakini, kujitolea na uzalendo wakati
wakitekeleza majukumu yao wanapowahudumia wananchi.
Wito
huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga wakati akifunga mafunzo
yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa madaktari na watoa
huduma za afya kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma ya namna ya
kufanya tathmini ya ulemavu (Impairment Assessment) kwa wafanyakazi walioumia
au kuugua kutokana na kazi.
“Mafunzo
mmeshapata, ninachofanya ni kukazia kwenye suala la integrity (uadilifu), seriousness
(umakini), commitment (kujitolea) na uzalendo, tunakwenda kufanya tathmini za
watu walioumia kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, anayestahili
fidia ndogo apewe fidia ndogo kulingana na ajali aliyopata na anayepata fidia
kubwa apewe fidia kubwa na usiangalie mtu aliyefika mbele yako ni wa aina gani.”
Alifafanua Dkt. Mganga.
Alisema
ni wajibu wa daktari kumdodosa mteja wake (mgonjwa) kwani itamsaidia kujua
historia yake na na hivyo kumuwezesha kujua kama tatizo lililomleta lina
uhusiano na kazi aliyokuwa akifanya au ni matatizo yaliyo nje ya kazi
anayoifanya.
“Kama
daktari hauko makini na kuwa mdodosaji (inquisitive) na ukienda juu juu mteja
(mgonjwa) atakudanganya, lazima ujue zaidi ya kile unachokiona machoni, hii
itakusaidia kutoa ripoti sahihi na hivyo kuuwezesha Mfuko kutoa Fidia Stahiki.”
Amesisitiza Dkt. Mganga, ambaye kitaaluma ni daktari wa binadamu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt.
Abdulsalaam Omar alisema mafunzo hayo yalihusisha madaktari 85 na hivyo kufanya
idadi ya madaktari waliopatiwa mafunzo kama hayo kufikia 1,386 nchi nzima.
Alisema
Mfuko umeweka mkazo mkubwa wa kutoa mafunzo kwa madaktari kote nchini ili
kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini ya ulemavu (Impairment Assessment) kwa
wafanyakazi walioumia au kuugua kutokana na kazi wakati akitekeleza majukumu ya
mwajiri kwa mujibu wa mkataba.
“Wenzetu
hawa madaktari ni daraja muhimu baina ya Mfuko na wafanyakazi, elimu hii
tuliyowapatia itawasaidia wafanyakazi wote watakaopita kwenye mikono yao kupata
matibabu stakihi lakini pia kupata fidia stahiki kwa mujibu wa sharia ya fidia
kwa wafanyakazi.” Alibainisha Skt. Omar.
Akizunhgumza
kwa niaba ya washiriki wenzake, Dkt.Nasibu Msuya kutoka Hospitali ya Rufaa ya
Kitete Mkoani Tabora aliushukuru Mfuko kwa mafunzo hayo kwani yamewapa uelewa
mkubwa wa jinsi Mfanyakazi anavyoweza kulipwa fidia pindianapopata matatizo
awapo kazini.
“Kazi
yetu kubwa ni kufanya tathmini ya ulemavu yaani Impairment assessment (kiwango
cha madhara aliyopata mfanyakazi) na disability (ulemavu) inafanywa na wataalamu
wa WCF wenyewe.” Alisema.
Alisema
mafunzo hayo yamewawezesha kujua taratibu zinazipasa kufuatwa kwa mfanyakazi
anayeumia au kuugua kitokana na kazi.
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga (kulia) akimkabidhi mmoja wa washiriki, Dkt. Nasibu Msuya cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar.