Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA)-Tanzania, Bi.Salome Kitomary akikata utepe kuzindua kampuni ya QM Beauty ambayo inajihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vipodozi vya asili pamoja na urembo kwa ujumla leo Oktoba Mosi, 2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA)-Tanzania, Bi.Salome Kitomary akipiga makofi baada ya kuzindua kampuni ya QM Beauty ambayo inajihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vipodozi vya asili pamoja na urembo kwa ujumla leo Oktoba Mosi, 2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA)-Tanzania, Bi.Salome Kitomary akizungumza katika uzinduzi wa kampuni ya QM Beauty ambayo inajihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vipodozi vya asili pamoja na urembo kwa ujumla leo Oktoba Mosi, 2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa QM Beauty,Bi.Saida Bandawe akizungumza katika uzinduzi wa kampuni ya QM Beauty ambayo inajihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vipodozi vya asili pamoja na urembo kwa ujumla leo Oktoba Mosi, 2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA)-Tanzania, Bi.Salome Kitomary akipata picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wadau mbalimbali wa kampuni ya QM Beauty katika uzinduzi wa kampuni hiyo ambayo inajihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vipodozi vya asili pamoja na urembo kwa ujumla leo Oktoba Mosi, 2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa na kampuni ya QM Beauty
*******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya QM Beauty ambayo inajihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vipodozi vya asili pamoja na urembo kwa ujumla imepongezwa kwa kufungua ofisi ambayo itaajiri vijana wengi wa kitanzania na kutatua changamoto za ngozi.
Pongezi hizo zimetolewa leo Oktoba 1,2022 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA)-Tanzania, Bi.Salome Kitomary wakati akifungua kampuni hiyo.
Ametoa wito kwa wajasiriamali na wawekezaji nchini kujifunza na kuona fursa za masoko duniani, “leo ifike wakati kampuni ya QM Beauty iwe na matawi katika nchi za Afrika Mashariki na SADC”.
Amesema Watu wengi wanapoanzisha jambo linapopata changamoto fulani wanakata tamaa na kuamua kuacha,lakini Mkurugenzi Saida hakukubali kikwazo kilichopo mbele yake,kila changamoto aliigeuza kuwa fursa.
“Nampongeza Mkurugenzi na timu yake kwa kutokukubali changamoto kuwa kikwazo cha kufikia malengo waliyokuwa wamejiwekea.Umetufundisha jambo kubwa sana”. Amesema Bi.Kitomary.
Amesema nchi zilizoendelea duniani hazitegemei ajira za serikali tu,bali sekta binafsi ndio inaendesha uchumi wa nchi na serikali inatengeneza mazingira mazuri ya kikodi,sheria na mambo mengine.
“Kama kuna changamoto zozote za biashara kustawi ni muhimu kupaza sauti ili serikali izisikie na kuzitatua,hivyo wajasiriamalu msikae kimya semeni kwa viongozi tuliowapa mamlaka”. Amesema
Aidha amesema Tanzania tuna bahati kwamba serikali ya sasa imeonyesha nia ya dhati ya kustawisha sekta binafsi,hivi karibuni tulimsikia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akielekeza kuangaliwa kwa sheria zote zinazokwaza uwekezaji,hivyo lengo ni kutaka sekta binafsi istawi na kuajiri watanzania wengi,ukiwa na sekta binafsi iliyostawi nchi inakuwa na uhakika wa kodi ambayo itakwenda kwenye huduma za kijamii na maendeleo ya watu moja kwa moja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa QM Beauty,Bi.Saida Bandawe amesema wameanza kampuni hiyo kutokana na changamoto zinazoikumba jamii hususani kwenye suala la ngozi kutokana na hali ya hewa pamoja na vyakula tunavyotumia.
“QM Beauty imefunguliwa kama mbadala wa kutatua changamoto zote kwa wababa na wamama wenye shida kwenye ngozi ambapo tunatoa ushauri kuhuu masuala ya ngozi na nywele na pia tunavipodozi asilia ambayo vinakua mbadala kwenye kutatua matatizo yao”. Amesema Bi.Bandawe
Amesema wamekuwa wakisaidia kutoa ajira kwa vijana kwa kuwapatia bidhaa hizo kwa bei ya jumla na kwenda kuanza biashara yake na wengine wamekuwa wakipatiwa ajira ndani ya ofisi ya QM Beauty.
Paamoja na hayo ametoa wito kwa vijana kufanya kazi kwa bidii na kuweza kusaidia jamii kwa ujumla.