********************
Katika kutekeleza adhima ya Mhe Rais Samia Suluh Hassan ambaye ni kiongozi wa machifu nchini Chifu ‘Hangaya’ ya kuuhuisha kuendeleza tamaduni za kichifu nchini, Hatimaye Chifu wa kabila la Wanyakyusa ,Chifu Edwin Mwakatumbula leo amekabidhiwa Ikulu yake ya Kichifu na kiongozi wa machifu wadogo wa kabila hilo.
Akizungumza katika tukio hilo la kihistoria, Chief Edwin amesema kuwa imekuwa siku ya baraka kwenye himaya hiyo, kwa yeye kukabidhiwa Ikulu hiyo iliyojengwa Mwaka 1900.
Aidha amesema kuwa kazi aliyokabidhiwa na machifu wadogo wa kabila hilo ataendelea kuifanya kwa kuzingatia mila na desturi za kabila hilo maarufu nchini.
Amesema kuwa aliporithi uchifu wa kabila hilo kutoka kwa marehemu Chifu Daudi B Mwakatumbula miaka 10 iliyopita amejitahidi kuendeleza mila za kabila hizo huku akidumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wanyakyusa wote nchini.
Chifu Edwin amesema kuwa ,jamii ya wanyakyusa nchini wanapaswa kujivunia hali ya amani na umoja miongoni mwao huku akihaidi kuendela kulilea kabila hilo kwa kuzingatia misingi na tamaduni zao.
Mbali ya kuwa Chifu, Edwin anahistoria kubwa kwenye siasa za nchi hii, huku akihudumu kwenye nafasi mbalimbali za kiungozi na kiutawala kwenye maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa nyakati tofauti amehudumu kama Katibu wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya wilaya ambapo mara ya mwisho alikuwa katibu wa chama wilaya ya Geita.
Chief Edwin ni miongoni mwa watoto 129 wa marehemu Chief Bentamanile Mwakatumbula wa kabila ilo ambaye alifariki dunia mwaka 1955 huku akicha wake 52 .
Vitabu vya kihistoria vya kabila la Wanyakyusa vinamtambua Chifu Bentamanile Mwakatumbula kwa mageuzi makubwa ya kiutawala aliyoyafanya wakati wa utawala wake wa miaka 45.
Katika kuthibitisha hilo, Alikuwa Chifu pekee kutoka Tanganyika aliyekabidhiwa Cheti cha heshima kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza.
Wakati wa utawala wake, alihesabiwa miongoni mwa machifu wa kimila waliokuwa mstari wa mbele kuipambania nchi uhuru, huku Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius K Nyerere akisema kuwa kazi kubwa waliyoifanya kipindi hiko katika Mikoa ya kanda za juu kusini hususani mkoa wa Mbeya zilikuwa za kutukuka na kurahisisha kuiunganisha nchi.