Dotto Mwaibale na Philemon Mazalla, Singida
TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imepeleka
teknolojia ya kilimo cha mazao mchanganyiko wilayani Iramba mkoani Singida ili
wakulima waweze kunufaika na kilimo.
Hayo yameelezwa na Meneja Uhaulishaji wa Teknolojia,
Biashara na Uhusiano wa taasisi hiyo, Margaret Mchomvu kutoka makao makuu ya
TARI Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa
kongamano la msimu wa kilimo 2022/2023 wilayani humo lililofanyika Septemba 28,
2022.
Alitaja bidhaa zilizotokana na teknolojia hiyo zilizooneshwa
katika kongamano hilo kuwa ni za mazao aina mbalimbali jamii ya nafaka kama
mtama, mahindi, uwele,ulezi na mazao aina ya mikunde ambayo yanastawi kwa wingi
mkoani Singida hasa wilayani Iramba.
Mchomvu alisema
mazao hayo ni aina ya mbaazi,mikunde, kunde zenyewe, choroko na mbaazi
za muda mrefu na muda mfupi, korosho, miche, mahindi aina ya Uchavuzi Huru (OPV) na
chotara ambayo wakulima wanaweza kuyanunua na mbegu za miti aina Lukina kwa ajili ya kuweza kuwaelimisha wakulima waweze kuzichagua kabla ya
msimu.
“Tumewaeleza wakulima kanuni ya kilimo bora ili wajue
umbali wa mche na mche na umbali kati ya mstari na mstari na namna ya kupanda
kwa utaratibu huo” alisema Mchomvu.
Alisema dhumuni la TARI ni kuona mkulima analima kilimo
chenye tija na bila ya kufanya kilimo hicho hata weza kuona faida ya kilimo na
kushindwa kufikia mkakati wa Serikali wa ajenda 10/30 kama wataendelea kulima
kilimocha mazoea.
Mtafiti wa kilimo kutoka kituo cha TARI, Tumbi Tabora,
Moses Adam alielezea teknolojia za Kilimo Misitu pamoja na uendelezaji wa mbegu
bora ambazo zinakingiza na wadudu, magonjwa huku zikihimili ukame na zenye tija..
Kwa upande wake Mtafiti wa kilimo Ramadhani Mlawa kutoka
Kituo cha Ilonga alipata fursa ya kuzungumzia mazao ya aina tofautitofauti ambayo wanayashughulikia zikiwemo mbegu za
alizeti, kunde mbaazi na nyingine nyingi ambazo zinatija na zinaweza kuhimiri
changamoto mbalimbali ya magojwa, ukame na baadhiya wadudu ambao wanashambulia
mazao.
Mlawa alitaja teknolojia zingine walizozionesha katika
kongamanohilo ni zile zinazotokana na mbegu zao kama vile unga wa mazao ya
mihogo, mtama, viazi na viazi vitamu ambao umechanganywa na choroko.
Alitaja vitu vingine kuwa ni biskuti, tambi, soya,bisi na
mafuta ya alizeti na kuwa wanaonesha vitu hivyo ili kuonesha mnyororo wa
thamani ikiwa ni kukamilisha ajenda ya Serikali ya 10/30 ambayo inasemakilimo
ni biashara.