Na
Fredy Mgunda, Iringa.
MKUU
wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametangaza vita na mwananchi yeyeto
anajihusisha na ujangiri wa wanyama pori katika hifadhi ya Taifa Ruaha hiyo
imetokana na kuongezeka kwa vitendo vya ujangiri katika Vijiji ambavyo
vinaizunguka hifadhi hiyo.
Akizungumza
wakati wa utiaji wa saini Mkataba wa makubaliano ya katika uhifadhi na
usimamizi, maendeleo ya jamii na kukutunza mali hai zote baina ya wananchi wa
Kijiji cha Kitisi na Lion landscapes katika kata ya Idodi wilaya ya Iringa,
Moyo alisema kuwa ujangiri umekuwa unaongezeka kila siku.
Moyo
alisema kuwa serikali itawafungulia mashitaka viongozi wa Serikali za
vijiji wakiwemo wenyeviti watakaozembea katika vita ya kutokomeza ujangili
katika maeneo yao huku akiwataka kuunda vikundi maalum vya ulinzi shirikishi.
Alisema
kuwa umeanza kuongezeka kwenye Vijiji ambavyo vinapakana na hifadhi ya Taifa
Ruaha kiasi kwamba kunahatarisha uhai wa wanyama pori ambao wamehifadhiwa
katika hifadhi hiyo.
Moyo
alisema kuwa serikali ya wilaya ya Iringa haitamfumbia macho mtu yeyeto yule
ambaye atakutwa na kesi ya ujangili basi ajue maisha yake yataishia Gerezani.
Aidha
mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliwapongeza Lion landscapes
kuendelea kuwalinda wanyama pori na kuviwezesha kiuchumi Vijiji ambavyo vipo
kwenye mradi huo.
Awali
meneja wa Mradi wa Lion landscapes Wiston Mtandamo alisema kuwa bado wananchi wa Kijiji cha Kitisi wanaendelea na ujangili
kwa kuuwa wanyama mbalimbali kwa ajili ya kupata kitoeo,kutumisha Milla na
wengi kwa ajili ya biashara haramu ya kuuza nyama pori mtaani kinyume na sheria
za nchi.
Mtandamo alisema kuwa kwa kipindi cha miezi
mitatu wamekamata mitego tisa ambayo ilikuwa imetegwa porini kwa ajili ya
kuwanasa wanyama pori Jambo ambalo linasababisha kutoweka kwa baadhi ya wanyama
pori.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya mapogolo Julias Mbuta amewahimiza wananchi wa
kijiji hicho na vijiji vyote vinavyounda kata ya Idodi kuhakikisha
wanashirikiana Mradi wa Lion landscapes na serikali katika kuendeleza uhifadhi
kwa manufaa ya Vijiji vyote vilivyo jirani na vilivyo nje ya hifadhi ya Taifa
ya Ruaha.