************************
29 September 2022
katibu wa Nec, Idara ya Organaizesheni CCM Taifa Dr. Maudline Castico ameshiriki na Kuchangia Mada katika Mdahalo wa wazee na Uzee uliofnyika Jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi ni Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kila tarehe 01 October ni wakati ambao Taifa la Tanzania tunatafakari maendeleo ya wazee na Uzee waliotetea na kuibua Changamoto kwa wazee na kushirikiana na Serikali kutatua Changamoto hizo .
Chama Cha Mapinduzi kinatambua Mchango Mkubwa wa wazee katika maendeleo ya kiuchumi katika Taifa la Tanzania, ndiyo maana Kuna Baraza la wazee wa CCM linalowakilisha wazee Nchi nzima ili kutekelaza Ilani ya CCM 2020 – 2025 katika kuleta Mabadiliko Makubwa kwa Wazee, na Uzee ni dawa Amesema Dr. Maudline Castico
Aidha Kwa kutambua Umuhimu wa wazee Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan sambamba na kutekeleza ilani ya CCM 2020 – 2025 inafanya Mchakato wa hatua ya Mwisho ya Rasimu ya Sera ya wazee kuwa Sheria. Amesema Dr. Maudline Cyrus Castico.
Mdahalo huo Umeratibiwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mzee Joseph Butiku.
Miaka 61 ya Uhuru, Tupo wapi na Tunakwenda wapi.