Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na Taarifa ya Tamasha la Maulid lenye lengo la kutoa Elimu ya namna ya kufurahia mazazi ya Mtume Muhamad (SAW)na namna inavyotakiwa kusomwa kwa Maulid,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika hafla ya utoaji taarifa ya Tamasha la Maulid lenye lengo la kutoa Elimu ya namna ya kufurahia mazazi ya Mtume Muhamad (SAW)na namna inavyotakiwa kusomwa kwa Maulid, iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali akijibu maswali alioulizwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na Taarifa ya Tamasha la Maulid lenye lengo la kutoa Elimu ya namna ya kufurahia mazazi ya Mtume Muhamad (SAW)na namna inavyotakiwa kusomwa kwa Maulid,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
……………………………….
NA SABIHA KHAMIS ,MAELEZO
Baraza la Maulid Zanzibar, limewataka wazanzibar wote kushirika katika maadhimisho ya Tamasha la Maulid ambalo litaambatana na maonesho kwa lengo la kuielimisha jamii.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Gwali ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema Tamasha hilo lina lengo la kuanzisha maonesho makubwa ya Kiislam katika kipindi cha sherehe za kuadhimisha uzawa wa Mtume S.A.W.
Amesema Tamasha hilo lina lengo la kuonesha namna bora ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad S.A.W kwa kuzingatia maadili na nidhamu ya Maulid ya Kiislam ambayo kwa miaka ya hivi karibuni imeanza kuondoka hivyo tamasha hilo limekuja kurejesha urithi wenye haiba na hadhi iliyoachwa na wanazuoni.
Aidha, amesema katika Tamasha la Maulid Zanzibar linatarajia kufanyika kwa matukio mbali mbali ikwemo maonesho ya Kiislam na biashara ambayo yafanyika kwa muda wa siku saba na kutarajiwa kuhudhuriwa na taasisi 40.
Vile vile, maonesho hayo yanatajiwa kufanyika kuanzia tarehe 03/10/2022 hadi 10/10/2022 katika uwanja wa Mapinduzi Square Kisonge na harakati mbali mbali za Kiislam zitaoneshwa na kutangazwa zikiwemo huduma za kibenk, Madrasa za Qur-an na harakati zao.
Hata hivyo, Kadhi huyo amesema kutakuwa na kongamano la wanawake na vijana ambayo yatahudhuriwa na wahadhiri mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo kuadhimisha uzawa wa Mtume Muhammad S.A.W.