*************************
Na Farida Mangube Morogoro
Mchezo wa kuvuta Kamba umetajwa kuwa miongoni mwa Michezo rahisi na muhimu katika kuimarisha afya hasa kwa wafanyakazi ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi wakiwa katika mjukumu ya kila siku huku wengine wakiwa wameketi.
Licha ya mchezo huo kutopewa nguvu kubwa na wadau wa michezo pamoja na Serikali kama ilivyo michezo mingine kama Mpira wa miguu, Pete, riadha na kuogelea lakini umekuwa kivutio Cha Watu wengi pale wanapoona watu mwenye Nguvu na miili Mikubwa wakivutana Kwa kutumia kamba .
Ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Bandari Inerport Games, katika viwanja vya Chuo kikuu cha waislam Morogoro, mchezo wa kuvuta kamba uliovuta hisia za wengi wakishangaa namna ya mchezo huo unavyochezwa na kikubwa zaidi ushindi unvyopatikana kwenye mchezo huo.
Abdallah Waziri Meneja wa Timu ya Kuvuta Kamba kutoka Bandari ya Tanga, miongoni pia mwa washiriki wa mchezo huo kwa zaidi ya miaka 10 na kwa sasa ana umri wa takribani miaka 57 lakini ni kati ya wanaofanya vizuri kwenye mchezo wa kuvuta kamba katika timu yake ya Bandari ya Tanga.
Waziri anaeeza Siri ya mafanikio yake kwenye mchezo huo kuwa ni mazoezi ambayo yamemfanya kuendelea kuwa na Afya Njema licha ya umri wake Mkubwa, ambapo aliwataka vijana hasa watumishi wa umma kufanya mazoezi pale wanapopata muda na sio kusubiri mpaka kipindi Cha mabonanza na mashindano yanayoandaliwa na Taasisi.
Kwa Upande wao baadhi ya washiriki wa mchezo huo akiwemo Siraji Yusuph na Halima Makame walisema mchezo wa kuvuta kamba, ni kati ya michezo rahisi kwani hutumia muda mfupi unaotumia nguvu lakini matokeo yake yanadhihirika hasa muonekano wa nje
Mishindano hayo ya 16 michezo ya Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania, inatarajiwa kufikia tamati Oktoba tatu mwaka huu wa 2022, mashindano yanayohusisha michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa kuvuta kamba