Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na walimu namna ambavyo ukatilii wa kingono unavyokuwa kwa kasi baina ya walimu na wanafunzi
Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Iringa vijijini Mwl Simoni Mnyawami akiongea jambo na Mwenyekiti wa Chama cha waalimu Mkoa wa Iringa Mwalimu Stanslaus Muhongole wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho wilaya ya Iringa Vijijini
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongongozwa na Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Iringa vijijini Mwl Simoni Mnyawami kutoka kwenye mkutano huo mara baada ya kumaliza kuhutubia
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akipokea hotuba ya walimu wa Iringa Vijijini wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA
Cha Walimu Wilaya ya Iringa vijijini (CWT) kimeonya kuwa hakitohusika na
utetezi Wa Waalimu watakaojihusisha na vitendo vya utovu Wa nidham ikiwemo
mahusiano ya kingono na wanafunzi.
Mwenyekiti Wa CWT
Wilaya ya Iringa Vijijini Mwalimu Simoni Mnyawami amesema ni aibu kusikia
waalimu wakitajwa kuhusika uhalifu huo huku akisisitiza hatua zaidi za kisheria
zichukuliwe ili iwe fundisho Kwa watakaobainika.
Mwenyekiti huyo ameyasema
hayo wakati wa mkutano mkuu wa CWT baada ya Mgeni wa Heshima mkuu wa wilaya ya
Iringa kuwataka waalimu kuzingatia weledi wa taaluma kwa kuwafifichua
wanaojihusisha kingono na wanafunzi.
Mnyawami alisema kuwa
suala la utovu wa nidhamu linapaswa kuheshimuwa kwa kila mwalimu ili kulinda
hadhi ya taaluma hiyo Ikiwemo Utoro, ulevi wa kupindukia pampja na baadhi ya
waalimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.
Mwenyeji wa Mkutano
Huu mkuu wa kikatiba Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Iringa vijijini Mwl Simoni
Mnyawami alisema ni muhimu waalimu akatambua na kuheshimu taaluma waliyo nayo
Kwa kuwa wamepewa dhamana na serikali pamoja na jamii kuwa walezi wa watoto
katika kuwajenga kinidham na kitaaluma
Kulingana na Changamoto
ya utovu wa nidham unaotajwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliyekuwa
Mgeni wa heshima anasema jambo la walimu kujihusisha kimapenzi na
wanafunzi halipaswi kufumbiwa macho
Moyo amewataka walimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wanaowafundisha ili taifa liweze
kupata wasomi wengi ambao wanauwezo wa kuja kukisaidia Taifa hapo baadae.
Alisema kuwa Kuna baadhi
ya walimu wamekuwa wakiaribu taswira halisi ya kada ya ualimu kwa baadhi ya
walimu kufanya mapenzi na wanafunzi na uwafanyia
ukatili wanafunzi kwa makusudi hivyo walimu wanapaswa kutoa taarifa kwa mwalimu
yeyeto atakayekutwa anafanya vitendo vya ukatili.
Alisema kuwa kazi kubwa
ya mwalimu ni kuwafundisha wanafunzi waweze kufaulu na sio kuwafanyia ukatili
wanafunzi..
Aidha Moyo alimazia kwa
kusema kuwa walimu wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa wamekuwa wanafanya vizuri
kwenye kufundisha wanafunzi ndio maana matokeo yake yamaekuwa mazuri mwaka hadi
mwaka.