Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Heri James ( mgeni rasmi) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya ” Asante Mwalimu” iliyozinduliwa na Benki ya Mwalimu leo Jumatano Septemba 28 Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha walimu wanakua na mazingira bora kwenye kazi yao.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Heri James akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampeni ya ” Asante Mwalimu iliyozinduliwa na Benki ya Mwalimu leo Jumatano Septemba 28 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya Mwalimu Leticia Ndongole akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampeni ya” Asante Mwalimu” iliyozinduliwa na Benki ya Mwalimu leo Jumatano Septemba 28 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Heri James akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya Mwalimu baada ya halfa ya uzinduzi wa kampeni ya” Asante Mwalimu” iliyozinduliwa na Benki ya Mwalimu leo Jumatano Septemba 28 Jijini Dar es Salaam.
*******************************
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha walimu wanakua na mazingira bora kwenye utoaji wa huduma kwa jamii na hata baada ya kustaafu Benki ya Mwalimu leo Jumatano Septemba 28 imezindua rasmi kampeni iitwayo “Asante Mwalimu”
Kupitia kampeni hiyo ya ” Asante Mwalimu” Benki hiyo inakwenda kutambulisha ” Bando la Mwalimu” ambalo ni mkusanyiko wa bidhaa mbalimbali zinazomlenga Mwalimu moja kwa moja zikiwa na lengo la kumpatia suluhisho la kifedha na kumlinda mwalimu na athari kubwa za mikopo umiza.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ( mgeni rasmi) amesema kuwa Serikali ina jukumu la msingi katika kuwajali na kuboresha mazingira ya walimu kwasababu mwalimu ni mtu pekee anayekaa na mtoto kwa muda mrefu na ana mchango mkubwa katika maelezi ya watoto.
Mkuu wa Wilaya hiyo ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Sekta ya elimu nchini kwa kujenga madarasa na kuboresha mazingira ya walimu wenyewe.
Hata hivyo Heri James ametoa wito kwa walimu kuchangamkia fursa ya huduma ya ” Bando la Mwalimu” kwakua ni huduma ya kipekee kuwahi kuzinduliwa hapa Nchini ambayo imelenga kumpatia suluhisho la kifedha Mwalimu.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya masoko Benki ya Mwalimu Retisia Ndombole amesema kuwa bando la Mwalimu linaenda kuwa suluhisho kwa Walimu ambao wamekua wanalipa riba kubwa na kupata mikopo umiza
” Bando la Mwalimu ni mkusanyiko wa bidhaa mbalimbali zinazomlenga Mwalimu moja kwa moja zikiwa na lengo la kumpatia la kifedha na zaidi kumlinda mwalimu na athari kubwa za mikopo umiza ambayo imeendelea kua kilio kikubwa kwa Walimu wetu” amesema
miongoni mwa bidhaa zitakazopatikana kwenye ” Bando la Mwalimu” ni pamoja na ‘Career Account’ , Mwalimu Jikimu, Ada chap chap, ‘Salary Advance’ , Mchongo fasta, ‘ ‘Mwalimu Personal Loan’, Mlinde mstaafu na ‘ Wastaafu Loan’.