Muogeleaji Lorita Borega (kulia) akipongezwa na baba yake mzazi Lameck Borega
Muogeleaji Lorita Borega katika pozi tofauti mara baada ya kuzawadiwa kikombe cha ushindi wa jumla katika mashindano ya wazi ya Taifa
………………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Muogeaji chipukizi wa klabu ya FK Blue Marlins Lorita Borega amevunja rekodi nne katika mashindano ya wazi yaliyomalizika hivi karibuni kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki.
Mbali ya kuvunja rekodi hizo, Lorita ambaye ilishinda afasi ya kwanza kwa waogeleaji wenye umri kuanzia miaka tisa (9) na 10 katika mashindano hayo baada ya kukusanya jumla ya pointi 116.
Vile vile, muogeleaji huyo anayesoma shule ya DIS, ameweza kushinda medali tano za dhahabu, moja ya fedha na kikombe baada ya kuwapiku waogekeaji wengine 16 katika mashindano hayo yaliyondaliwa na Chama Cha Kuogelea Tanzania(TSA).
Akizungumza mara baada ya mashindano hayo kumalizika, Lorita alisema kuwa amejisikia faraja kubwa kuibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo huku ikiwa ni mara yake ya pili kushiriki.
“Mashindano yalikuwa magumu na kila muogeaji alikuwa anawania nafasi ya kwanza, namshukuru Mungu kwa mafanikio niliyopata na sasa nina wapa pongezi makocha wangu, wazazi wa klabu ya FK Blue Marlins, waogeaji wenzangu na wazazi wangu kwa kunipa sapoti kubwa,” alisema Lorita ambaye anasoma darasa la sita katika shule ya DIS.
Muogeleaji huyo aliweza kushinda medali katika shindano la mita 50 katika mtindo wa butterfly, mita 100 (butterfly), mita 50 (freestyle), mita 100 (Individual Medley) na mita 100 katika mtindo wa freestyle.
Pia alishinda medali ya fedha katika mtindo wa breaststroke katika mita 50.
Lorita pia alivunja rekodi na kuweka mpka katika staili ya butterfly ya mita 50 kwa kutumia muda wa 35.27 kuiondoa rekodi ya Sydney Hardeman aliyoiweka mwaka 2018 kwa kutumia muda wa sekunde 37.38.
Pia alivunja rekodi na kuweka mpya katika staili ya butterfly kwenye mita 100 kwa kutumia muda mpya wa wa dakika 1.23.60 na kuiondoa rekodi ya Sydney aliyoiweka mwaka 2018 ya muda wa 1.24.24.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Lorita alivunja rekodi ya mita 50 katika staili ya freestyle kwa kuweka muda wa 32.62 na kuifuta rekodi ya Crissa Dillip ya skunde 32.72 na vile vile kuifuta rekodi nyingine ya Crissa ya dakika 1.11.62 kwa kutumia muda mpya wa dakika 1.11.60 katika mtindo wa freestyle. Crissa aliweka muda huo mwaka 2021.