Mkuu wa Kitengo cha mauzo Benki ya Letshego Leah Phili akizungumza na Waandishi wa habari wakati akitangaza huduma mpya mbili za akaunti ya Benki hiyo ambazo ni Akaunti ya Mjasiriamali na Akaunti ya Mstaafu Leo Jumanne Septemba 27 Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Kitengo cha masoko Benki ya Letshego Uswege Mwaipyana akizungumza na Waandishi wa habari wakati akitangaza huduma mpya mbili za akaunti ya Benki hiyo ambazo ni Akaunti ya Mjasiriamali na Akaunti ya Mstaafu Leo Jumanne Septemba 27 Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam.
************************
Benki ya Biashara ya Letshego ambayo ipo Sokoni tangu mwaka 2016 leo Jumanne Septemba 27, 2022 imetangaza kuzindua huduma mpya mbili za akaunti ambazo ni akaunti kwaajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati ( Mjasiriamali Account) na akaunti ya Wastaafu ( Mstaafu account)
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Septemba 27 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha mauzo Benki ya Letshego Leah Phili amesema huduma ya akaunti ya wajasiriamali ni kwaajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati ambayo itakua inawawezesha kuweka akiba zao wakiwa na malengo maalumu kwenye Biashara zao .
Amebainisha kuwa huduma hiyo imelenga hadi wajasiriamali wadogo na wa chini kabisa ambao hawana nyaraka kama vile leseni na namba ya utambulisho ya mlipa kodi (Tin namba).
Ameongeza kuwa katika huduma hii ya akaunti ya Mjasiriamali wameondoa baadhi ya vitu ambavyo vitamfanya mteja ashindwe kupata huduma nzuri za kiakaunti ambapo amebainisha kuwa mteja anaweza kufungua akaunti ya Mjasiriamali kwa shilingi elfu moja(1000) ya kitanzania kwa kuanzia.
” Unaweza kufungua akaunti kwa shilingi 1000 na kutoa pesa hadi kiwango cha shilingi elfu kwa njia mbalimbali kama vile dirishani katika matawi ya Benki zetu, mifumo ya Kidigitali ambayo mteja anaweza akafanya miamala yake ” amesema Leah
Kwa upande wa akaunti ya Mstaafu Leah amesema walengwa ni wastaafu ambao wanaweza kufungua akaunti wakati wowote wakati wanajiandaa kustaafu na baada ya kustaafu.
Ameongeza kuwa sifa kubwa ya akaunti ya mstaafu ni kwamba haina makato ya mwezi ni akaunti ya bure na inahudumiwa bure na mstaafu anaweza kuweka kuanziaa elfu moja na kutoa hadi shilingi elfu moja.