WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa elimu wa Tanzania ikiwemo timu kutoka Zanzibar inayofanya mapitio ya sera na mitaala ya elimu,utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdulgulam Hussein,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa elimu wa Tanzania ikiwemo timu kutoka Zanzibar inayofanya mapitio ya sera na mitaala ya elimu,utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa elimu wa Tanzania ikiwemo timu kutoka Zanzibar inayofanya mapitio ya sera na mitaala ya elimu,utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa elimu wa Tanzania ikiwemo timu kutoka Zanzibar inayofanya mapitio ya sera na mitaala ya elimu,utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda,(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa elimu wa Tanzania ikiwemo timu kutoka Zanzibar inayofanya mapitio ya sera na mitaala ya elimu,utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda,akiwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdulgulam Hussein wakifatilia majadiliano wakati wa Mkutano wa Wadau wa elimu wa Tanzania ikiwemo timu kutoka Zanzibar inayofanya mapitio ya sera na mitaala ya elimu,utafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 26,2022 jijini Dodoma.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda,amesema kuwa wamekutana na wadau wa elimu nchini ili kujadili rasimu ya mapitio ya sera na mitaala kwa kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakikusanya maoni.
Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu jijini Dodoma kuanzia leo Septemba 26 hadi septemba 28, mwaka huu ambapo wadau hao na Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia watajadili maoni yaliyotolewa kuhusu masuala ya sera na mitaala nchini
Prof .Mkenda amesema kuwa kikao hicho ni kutekeleza Agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania samia suluhu hassani ambapo Mnamo Tarehe 22 April 2022 Bungeni alisema kufanyike marekebisho ya sera ya Elimu ya mwaka 2014 pamoja na mitaala iliyopo kwa maslahi ya Taifa na Watu wake.
“Kwa mara ya kwanza tunakutana kujadili tukiwa na rasimu,ya sera na mitaala, kwa muda mrefu tumekuwa tukikutana na kukusanya maoni sasa timu zetu zinazopitia sera na mitaala zina rasimu, kwa hiyo tuna kitu cha kufanyia majadiliano yetu,”amesema Prof.Mkenda
Prof.Mkenda amesema kuwa huwezi kuzungumzia ubora wa elimu bila kufanya mageuzi na mabadiliko katika sera na mitaala ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Dunia kwani kwa sasa taaluma na ujuzi zinakwenda sambamba.
“Tunapokwenda kufanya mageuzi ya elimu ni lazima twende na adhma ya Mhe.Rais aliyeagiza kuwa mbali tu na kujikita katika elimu ya taaluma tujikite pia katika Ujuzi hivyo ni lazima tuhakikishe tunatoa mawazo ambayo itasaidia kuboresha elimu yetu sio kushusha ubora,”Amesema Prof.Mkenda
Na kuongeza kuwa “Swala la elimu sio la Tanzania peke yake ni la kidunia hivyo lazima tufanye mageuzi ili kuendani na kasi ya mabadiliko katika sekta ya elimu duniani,”Amesema
Waziri Mkenda amesema kuwa wadau wataangalia gharama za kufanya mageuzi kwenye mitaala na sera.
“Tutaambiwa tunahitaji kuwa na walimu wangapi ili tunapofanya mabadiliko tujue tunatumia njia gani kuboresha idadi ya walimu na vitendea kazi,”amesema.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein, amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa hatma ya maendeleo ya nchi kwa kuwa watakapokosea sera na mitaala watakuwa wamelikosea taifa.
“Najua mtafanya mapitio ya sheria kuunga mkono utekelezaji wa sera, haina maana kwamba nchi yetu haina sera au mitaala bali vyanzo hivi lazima vifanyiwe mapitio au kuangaliwa upya baada ya muda fulani kutokana na ukubwa wa mabadiliko yanayotokea nchini na duniani kwa ujumla.”amesema
Naye, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema suala la mapitio ya sera na mitaala lina hamu kubwa kwa watanzania kutokana na maswali yanayoulizwa bungeni na wabunge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar, Abdallah Mohamed Mussa, amesema kutokana na mabadiliko yanayoendelea sayansi na teknolojia bado sera zitanakiwa kuboreshwa hasa mtoto anapomaliza elimu ya lazima kuonyesha viashiria vya kujitegemea.
“Hakukuwa na mapungufu makubwa, (sera), isipokuwa ni kuonyesha uwazi kwa elimu inayotolewa ukianza na elimu ya lazima anapomaliza elimu hiyo ni skill (ujuzi) gani mataupata huyo mwanafunzi, ndicho kinachokwenda kuwekwa bayana,”ameeleza