Na John Walter-Babati
Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Babati mjini imepata viongozi wapya wa jumuiya ya wazazi watakao iongoza jumuiya hiyo kwa miaka mitano ijayo.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi Muna Siay amemtangaza Emanuel Qambay kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Babati mjini kwa jumla ya kura 112, nafasi ya uwakilishi UVCCM wilaya mshindi ni Amina Hassan Juma kwa jumla ya kura 116, nafasi ya uwakilishi umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi kwa ngazi ya wilaya mshindi ni Rukia Juma Mohamed kwa jumla ya kura 164.
Nafasi ya mkutano mkuu wazazi mkoa mshindi ni Ismail Iddy Mshana kwa jumla ya kura 146, nafasi ya uwakilishi mkutano mkuu taifa mshindi ni Wilhelmo Mayo kwa jumla ya kura 117, nafasi ya uwakilishi baraza la wazazi wilaya inayojumuisha wawakilishi watatu na washindi ni Prosper Paulo Yahi kwa jumla ya kura 69, Jumanne Hassan Dudu kwa jumla ya kura 95 na Rukia Waziri kwa jumla ya kura 129.
Nafasi ya mkutano mkuu CCM mkoa mshindi ni Bonifas Justin kwa jumla ya kura 93 na nafasi ya mjumbe wa halmashuri kuu CCM na mjumbe wa mkutano mkuu CCM wilaya mshindi ni Wilhelmo Mayo kwa jumla ya kura 128.
Baada ya matokeo hayo kutangazwa mshindi wa nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Emanuel Qambay alipata wasaa wa kutoa shukrani kwa wajumbe wote waliopiga kura na kuwaomba ushirikiano katika utendaji wa majukumu mbalimbali katika jumuiya hiyo, ili isonge mbele na kuahidi kutatua changamoto zote zilizojitokeza katika uongozi uliopita. Na baada ya kumaliza kutoa shukrani akafunga mkutano hadi wakati mwingine watakapo kutana tena kwa shughuli mbalimbali za jumuiya hiyo ya wazazi.