Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuanzia Septemba 18, 2022 hadi Septemba 25, 2022 limefanya misako ya nguvu ya yenye tija katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya na kupata mafanikio ikiwemo kukamatwa kwa watuhumiwa 23 kati yao watuhumiwa 02 wa wizi wa Pikipiki, watuhumiwa 04 wezi na matapeli wa mitandaoni, watuhumiwa 03 wezi wa magari, watuhumiwa 07 wauzaji wa Pombe haramu ya Moshi na watuhumiwa 06 wa Dawa za Kulevya aina ya Bhangi.
WANNE WANASHIKILIWA KWA WIZI KWA NJIA YA MTANDAO.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana wanne [04] wakazi wa Mji Mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma za utapeli na wizi kwa njia ya mtandao kwa kutumia majina ya watu maarufu na kuwaahidi kutoa ajira za vyombo vya usalama ikiwemo Polisi na JKT na kutoa mikopo kwa gharama nafuu.
Katika misako iliyofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya katika Mji mdogo wa Mbalizi lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne [04] ambao ni:-
- EZECKIA SIMON [19] Mkazi wa Shigamba
- AMASHA MERNAD MBEYALE [24] Mkazi wa uwanja wa Maubili,
- SHABANI AMIDU [28] Fundi rangi, Mkazi wa Mwakapangala,
- BENNY JULIAS SANGA [28] Mkazi wa Ndola
Watuhumiwa wamekuwa wakiwatapeli na kuwaibia watu kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya “Facebook” kwa kutengeneza machapisho ya uongo kwa madai kuwa wanatoa mikopo kwa gharama nafuu na kuwa wanatoa ajira kwa kutumia majina na picha za watu maarufu, Nandy na Jokate Mwegelo.
Aidha watuhumiwa wamekuwa wakiwatapeli na kuwaibia watu kwa kutuma jumbe fupi za maneno “Nafasi za kazi za JKT kama una mtoto wako wasiliana nasi” Pia ujumbe unaosomeka “Tuma pesa kwenye namba hii”
Watuhumiwa wamepekuliwa kwa mujibu wa sheria na kukutwa na vitu mbalimbali:-
- Laini za mitandao mbalimbali 36 zenye majina na umiliki wa watu wengine.
- Simu za mkononi 07 za aina mbalimbali wanazozitumia kuwaibia watu.
- Nyaraka mbalimbali.
- Picha mbalimbali.
- Machapisho mbalimbali.
Watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KUKAMATWA WATUHUMIWA WA MTANDAO WA WIZI WA MAGARI MBEYA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya hivi karibuni limeendesha operesheni na misako katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya dhidi ya wahalifu wa wizi wa magari. Katika Operesheni na misako hiyo, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata magari yaliyoibwa sita [06] na watuhumiwa wa mtandao wa wizi wa magari watatu [03].
Watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na:-
- YUSUPH OMARY RAMADHANI [26] Mkazi wa Forest Jijini Mbeya.
- SHUKU JOSEPH NYEMA [23] Mkazi wa Songea Mkoa wa Ruvuma.
- ABUU NOELY RUTAGALAMA [26] Mkazi wa Itezi Jijini Mbeya.
Magari yaliyoibwa na kupatikana ni:-
- 795 DEX aina ya Prado TX rangi ya Silver ambalo lilisafirishwa mpaka nchini Malawi.
- 841 DYD Toyota Passo rangi nyekundu.
- 786 DLD Toyota IST.
- 649 DMH Toyota IST.
- Toyota IST isiyo na namba za usajili,
- Toyota SPACIO isiyo na namba za usajili.
Mnamo tarehe 14/09/2022 huko Mtaa wa Ikhanga, Kata ya Iganjo, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya AGNES AZIZI CHAULA, Mfanyabiashara, Mkazi wa Ikhanga akiwa anaendesha Gari yake lenye namba za usajili T.841 DYD Toyota Passo akitokea dukani kwake maeneo ya Uyole baada ya kufika getini nyumbani kwake alivamiwa na watu wawili na kumnyang’anya Gari hilo na kutokomea nalo.
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilianza ufuatiliaji na mnamo Septemba 18, 2022 Gari hilo lilipatikana huko katika pori la hifadhi ya Msitu wa Kijiji cha Ikoho uliopo Kata ya Maendeleo, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya vijijini. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na msako wa kuwabaini na kuwatia mbaroni watuhumiwa.
Taratibu za kuwakabidhi wamiliki wa gari hizo unaendelea.
KUKAMATWA WATUHUMIWA WA MTANDAO WA WIZI WA PIKIPIKI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. SAMWEL WISTON MWAMPANGATA [27] Mkazi wa Ngonga Wilaya ya Kyela na 2. YONA SABELI [46] Mkazi Mbegele kwa tuhuma ya wizi wa Pikipiki mbili.
Watuhumiwa kwa nyakati tofauti walikamatwa na kukutwa na Pikipiki za wizi MC 808 DHR aina ya Bajaji Boxer yenye Chassis namba MD2-A21-BX8NWL-98376 ambayo mtuhumiwa SAMWEL WISTON MWAMPANGATA [27] alikuwa katika harakati ya kuisafirisha kwenda kuuza nje ya nchi – Malawi. Pikipiki hiyo imetambuliwa na mmiliki aitwaye ELIEZA SADICK MWANDAGANI [18] Bodaboda, Mkazi wa Serengeti- Kyela.
Aidha mtuhumiwa YONA SABELI [46] alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za kuvunja Stoo na kuiba Pikipiki STL 8531 yenye Chasis namba LBPKE135600069064, Engine namba JYM154FM119102163 aina ya Yahama mali ya mamlaka ya bonde la ziwa nyasa. Pikipiki hii alikamatwa nayo akiwa tayari amefungua namba za usajili na kutenganisha baadhi ya vifaa ili kurahisisha kuisafirisha kwenda kuiuza.
WASHIKILIWA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI @ GONGO.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa saba [07] kwa tuhuma ya kupatikana na Pombe Haramu ya Moshi @ Gongo kiasi cha lita Arobaini na mbili [42] pamoja na mitambo ya kutengenezea pombe hiyo haramu.
Watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na:-
- VICTORY TULO MWAMBOLA [34] Mkazi wa Lubele.
- REGINA KANIKI [60] Mkazi wa Kibisi
- MUSA MWAMBANE [33] Mkazi wa Mwakaleli
- ANTONY MWAKALINDILE [46] Mkazi wa Kibisi
- SHABANI AFWENE [40] Mkazi wa Katumba,
- CATHERINE ASAJILE [39] Mkazi wa Kibisi
- TUNSUME IKEMBA [23] Mkazi wa Kasanga
Watuhumiwa walikamatwa wakiwa wanatengeneza, wanauza na kunywa Pombe hiyo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.
SITA WANASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa sita [06] kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bhangi.
Watuhumiwa waliokamatwa katika misako inayoendelea ni pamoja na:-
- EZECKIA SIMON [19] Mkazi wa Shigamba
- LEONARD BANGILE [25] Mkazi wa Shizya – Chunya
- SHUKURU SIMON MSOMBA [37] Mkazi wa Lubele
- DASTANI BUKA MASAPE [23] Mkazi wa Lubele
- FRANK SANGA [34] Mkazi wa Mapelele.
- PILISON FREDY @ MWASHIUYA [42] Mkazi wa Kasanga.
Watuhumiwa walipekuliwa na kukutwa wakiwa na dawa za kulevya aina bhangi zenye uzito wa kilogramu kumi [10] na gramu 395 pamoja na misokoto 78. Aidha watuhumiwa walikutwa na mbegu za mmea haramu wa bhangi. Watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
AKAMATWA AKIWA NA MALI MBALIMBALI ZA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia RONESHIA DAUD [28] Mkazi wa Mbalizi II kwa tuhuma za kujihusisha na matukio mbalimbali ya kuvunja nyumba usiku na kuiba katika mji mdogo wa Mbalizi na maeneo mengine ya Jijini Mbeya.
Mtuhumiwa alikamatwa na alipopekuliwa alikutwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-
- Laptop moja aina Samsang,
- Aplifaya moja,
- Radio ndogo moja
Mali zote zimetambuliwa na mlalamika ndugu KENEDY LETINI na taratibu za kumkabidhi kwa mujibu wa sheria zinaendelea. Mtuhumiwa anategemea kufikishwa mahakamani.
KAMPENI YA KUSALIMISHA SILAHA HARAMU KWA HIARI.
Mnamo tarehe 22/09/2022 silaha moja aina ya Shotgun yenye maker’s namba 36629, CAR namba 20858 pamoja na risasi zake tano ilisalimishwa katika kituo cha Polisi Kyela na mmoja wa wananchi wa Wilaya hiyo kufuatia elimu na matangazo mbalimbali ya usalimishaji silaha kwa hiari yanayoendelea kutolewa na wakaguzi Kata. Awali silaha hiyo ilikuwa ikimilikiwa kihalali na baba yake mzazi ambaye kwa sasa ni marehemu na kwa kipindi chote baada ya kufariki hakujua nini cha kufanya hadi pale aliposikia matangazo ya kusalimisha silaha kwa hiari ndipo alichukua hatua za kuipelekea kituo cha Polisi Kyela.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Benjamin Kuzaga anatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwabaini wahalifu kwenye maeneo yao ili kuweza kuondoa hali ya uhalifu. Pia anawataka wananchi kufika vituo vya Polisi kutambua mali zilizokamatwa na pia kushiriki kutoa Ushahidi mahakamani ili kesi zipate mafanikio kwa kiasi kikubwa.
Aidha nitumie nafasi hii kuendelea kuwaomba wakazi wa Mbeya kuendelea kusalimisha silaha katika vituo vya Polisi vilivyopo jirani nao, ofisi za serikali za mitaa, vijiji na kata katika kipindi kilichowekwa na serikali cha kuanzia Septemba 01, 2022 hadi Oktoba 31, 2022.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na misako mbalimbali ya kuwakamata wahalifu wa matukio mbalimbali na kuwachukulia hatua za kisheria.