NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA
MKUU
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema hivi sasa wafanyakazi wanao
uhakika wa kinga na kipato kutokana na majanga yanayosababishwa na ajali,
magonjwa na vifo kutokana na kazi kufuatia uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa
wafanyakazi (WCF).
Mhe.
Senyamule ameyasema hayo jijini Dodoma Septemba 26, 2022 wakati akifungua
mafunzo ya tathmini za ulemavu uliosababishwa na ajali na magonjwa yatokanayo
na kazi kwa madaktari wa mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma.
“WCF
ndio inayobeba jukumu la gharama zote pindi Mfanyakazi anapoumia, kuugua ama
kufariki kutokana na kazi.” Alifafanua.
Aidha
Waajiri nao wanapata muda zaidi wa kushughulikia uzalishaji na uendelevu wa
biashara zao na hivyo kuongeza tija inayopelekea kuongezeka kwa pato la taifa.
Alisema
uwepo wa Mfuko wa Fidia ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo
serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Samia Suluhu Hassan,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na kazi ikiwemo ya kujenga
uchumi na hivyo kuwa na ongezeko kubwa la maeneo ya uzalishaji.
“Katika
hali ya kawaida ongezeko litakwenda sambamba na ongezeko la matukio na athari
zinazotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi hivyo jukumu la WCF sio
kulipa Fidia pekee bali pia kushirikiana na wadau katika kubuni na kuendeleza
mbinu za kupunguza au kuzuia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.”
Alisisitiza.
Aliwaasa
washiriki kuwa waadilifu wanapotekeleza jukumu hilo la kufanya tathmini ya
ulemavu utokanao na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi ili WCF iweze kutoa
fidia stahiki na kwa wakati.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John
Mduma, amesema Mfuko unajivunia kufanya vizuri katika uboreshaji wa mifumo ya
kielektroniki ya utoaji huduma pamoja na punguzo la kiwango cha uchangiaji kwa
sekta binafsi kutoka asilimia 0.6% hadi 0.5% vilevile punguzo kubwa la riba
(interest) kwa madeni ya michango ya nyuma.
Alisema
Maboresho hayo yanalenga kukuza uzalishaji ambapo sasa Waajiri wa Sekta binafsi
wamepewa nafuu kubwa ya kuelekeza nguvu katika uzalishaji mali, huku WCF
ikiendelea kulinda nguvukazi ya Taifa.
“Kama
unavyofahamu tayari kuna mabadiliko makubwa sana ya uboreshaji wa mazingira ya
uwekezaji na biashara hapa nchini ndani ya kipindi cha Serikali ya awamu ya
sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, na sisi kama Mfuko tayari tumejipanga kuhakikisha tunaendelea kutoa
huduma bora wakati wote.” Alisema Dkt. Mduma.
Ameishukuru
Serikali na taasisi zake kwa namna inavyosaidia katika kuhakikisha Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi unaweka misingi imara katika kutekeleza majukumu yake
ipasavyo.
Aliwakumbusha
Waajiri kutumia fursa hii adhimu ya punguzo iliyowezeshwa na Serikali sikivu ya
Awamu ya Sita Ili kuongeza uzalishaji na hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Akizungumzia
kuhusu mafunzo hayo ya alisema yameandaliwa na WCF kama sehemu ya hatua muhimu
kuuwezesha kutekeleza vyema jukumu la kufanya tathmini sahihi na hatimaye Fidia
stahiki pindi mfanyakazi anapoumia au kuugua kutokana na kazi.
Uelimishaji
wa aina hii ni moja ya mikakati ya kuondoa changamoto ambazo zinaukabili Mfuko
mpaka sasa, kwani Mfuko unatambua umuhimu wa Mafunzo haya kwa Wataalamu ili
kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na uweledi wa hali ya juu na
hatimaye kusaidia Mfuko kutimiza lengo lake la kutoa fidia stahiki na kwa
wakati.