Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York
Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Ali Suleiman (wa tatu kulia) akizungumza katika kikao cha Mhe Waziri Mulamul alipokutana na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York
****************************
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York na kuwataka kutanguliza uzalendo na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa faida ya nchi.
Balozi Mulamula pia amewataka watumishi hao kusimamia matumizi mazuri ya fedha za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwenye vituo vya uwalikishi wa nchi na kutangaza kazi mbalimbli zinazofanywa na ubalozi ili kuonesha kazi zao na hivyo kuonesha umuhimu wa uwakilishi katika Umoja wa Mataifa na mchango wao katika Diplomasia ya Uchumi.
“Hapa New York mna kila sababu ya kujitangaza, nyinyi hapa mnamuingiliano mkubwa, ni nyumbani kwa Umoja wa Mataifa, lazima muoneshe faida ya nyinyi kuwakilishaa nchi kwenye Umoja wa Mataifa, onesheni mchango wenu katika shughuli za diplomasia ya uchumi na mashirika ya kimataifa,”alisema Balozi.
Amewapongeza kwa namna mnavyoshirikiana na Diaspora wa Tanzania walioko jijini New York, na kuawataka waendeleze ushirikiano huo kwani wao ni walezi na wasaidizi wao panapohitajika jambo la kufuatilia
Nimeona mna ushirikiano sana na Diaspora wa hapa, muendelee kuwashirikisha na muendelee kuwa walezi, washauri na msimbague mtu, sisi kama Wizara tunapenda kuwaona mkiwa pamoja, mshirikiane na Idara ya Diaspora katika kutekeleza suala hilo,” alisema Balozi Mulamula